• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Divisheni na Vitengo
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TASAF
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Usimamizi wa Usafi na Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha mawasiliano Serikalini
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2024-2025
      • Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

WATOTO CHINI YA MIAKA MITANO WAANZA KUPATIWA VYETI VYA KUZALIWA BURE BAGAMOYO

Posted on: December 6th, 2019

WATOTO WENYE UMRI CHINI YA MIAKA MITANO KUPATIWA VYETI VYA KUZALIWA BURE BAGAMOYO

Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, imeanza utekelezaji wa zoezi la usajili na utoaji vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano kuanzia leo tarehe 06 – 19/12/2019.

Zoezi hili limezinduliwa rasmi na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Mhe. Zainab Kawawa katika kliniki ya Mama na mtoto ya Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo (RCH) mapema leo asubuhi.

Akizungumza katika uzinduzi huo Mhe. Zainab amesema ni haki ya kila mtoto kupata cheti cha kuzaliwa, hivyo ni wajibu wa kila mzazi kuhakikisha mtoto wake anapata cheti cha kuzaliwa na katika kufanikisha hilo, ni vema wazazi kutumia fursa hii kuwasajili watoto wao walio chini ya umri wa miaka mitano ili wapatiwe vyeti vya kuzaliwa.

“Ni matumaini yangu kuwa kampeni hii itakuwa shirikishi, Mzazi ukipata cheti cha mwanao cha kuzaliwa, ukienda nyumbani usikifiche, nendeni mkawe mabalozi wazuri kwa wazazi wengine, kawaambieni kuwa vyeti vimeanza kutolewa bure kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano ili wengine pia wafike kusajili watoto wao na kupatiwa vyeti hivi vya kuzaliwa na hatimaye, kila mtoto anayelengwa katika mpango huu apate cheti cha kuzaliwa” Amesema Mhe. Zainab.

Nae Bi. Zuwena Selemani mmoja wa wazazi aliyefanikiwa kufanya usajili wa mtoto wake leo katika kituo cha usajili cha Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo, na binti yake Prisca Denis kupatiwa cheti cha kuzaliwa, ameishukuru Serikali kwa kuleta mpango huu karibu na wananchi kwani ni msaada mkubwa kwa wananchi wa Bagamoyo na kuongeza kwamba, ni hakika sasa kuwa kila mtoto aliye chini ya miaka mitano atapata cheti cha kuzaliwa kwa urahisi tena katika eneo analoishi.

Mpango wa usajili na utoaji vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano, utatekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo kwa muda wa wiki mbili kuanzia leo tarehe 06/12/2019 na utakamilika tarehe 19/12/2019, na baada ya hapo huduma hii itaendelea kutolewa katika vituo vyote vya kutolea huduma za Afya vya Serikali kwa kila mtoto atakayezaliwa katika vituo hivyo.

Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo imejiwekea lengo la kusajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa jumla ya watoto 14,565 kupitia mpango huu unaotekelezwa na Serikali ya Tanzania ikishirikiana na Serikali ya watu wa Canada, Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia watoto (UNICEF), Kampuni ya mawasiliano ya Tigo na Wakala wa Usajili, ufilisi na udhamini (RITA)





Matangazo

  • TANGAZO LA KUTEULIWA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 AWAMU YA PILI... May 09, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA BAGAMOYO... February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA OBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.. February 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI... July 14, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • HALMASHAURI YA BAGAMOYO YAPANDA MITI 500 ENEO LA MNADA WA ZINGA KUBORESHA MAZINGIRA...

    April 15, 2025
  • TUTAENDELEA KUSIMAMIA KWA DHATI NA HAKI MISINGI YA DEMOKRASIA...

    April 02, 2025
  • ELIMU KUHUSU MPOX YATOLEWA KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI...

    March 20, 2025
  • WAPENI ELIMU WANANCHI KUHUSU UGOJWA WA MPOX...

    March 17, 2025
  • Angalia zote

Video

SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 0733860575

    Simu ya kiganjani: 0733860575

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo