• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Divisheni na Vitengo
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TASAF
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Usimamizi wa Usafi na Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha mawasiliano Serikalini
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2024-2025
      • Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

WAZEE NI TUNU, TUWALINDE

Posted on: October 1st, 2020

Kila ifikapo Tarehe 01, Oktoba, Dunia huazimisha siku ya Wazee Duniani, na kwa Mwaka huu kauli mbiu inayobeba maadhimisho hayo inasema “Familia na jamii tuwajibike kuwatunza wazee”

Mratibu wa tathmini na ufuatiliaji wa taasisi isiyo ya Kiserikali ya ‘Help Age Tanzania’ Bi. Martha Kihampa ambaye alikuwa Mgeni mwalikwa akizungumza katika hafla hiyo amesema Wazee ni Tunu hivyo jamii ina wajibu wa kuwalinda na kuwatunza kama kauli mbiu ya Mwaka huu inavyoelekeza ili waishi kwa Amani na wafurahie uzee wao kwa kuamini kuwa jamii inayowazunguka ni msaada kwao na ipo tayari kuwalinda, kuwasaidia na kuwatetea wakati wote ili waishi maisha salama.

“Wazee wetu ni tunu yetu, ni kisima cha busara na viongozi wetu wanaoweza kutuelekeza namna bora ya kuishi na kufanya maamuzi sahihi yatakayoleta matokeo chanya katika jamii yetu, hivyo tuna wajibu wa kuwalinda na kuwatunza” Amesema Bi. Martha

Anaongeza, Idara ya Afya tunawaomba sana mtusaidie, anzisheni dirisha la kuhudumia wazee na wazee wawekewe bajeti inayojitegemea ya ununuzi wa dawa zao za matibabu ya wazee, hakikisheni mnawapatia huduma rafiki za Kiafya wakati wote wanapofika katika Vituo vya kutolea huduma za Afya kupata huduma, Viongozi wa Hospitali ya Wilaya na vituo vingine vya kutolea huduma ya Afya, sisitizeni lugha nzuri kwa wazee na ni vyema kitengo cha ustawi wa jamii kuanza taratibu za kuunda mabaraza ya wazee katika kila Kata kwani huko ndiko wazee wanaweza kukaa na kupaza sauti kusema mahitaji yao na kupata ufumbuzi wa matatizo yao, pia kubadilishana mawazo na kufanya mazoezi na kushiriki michezo mbalimbali itakayowaburudisha pia.

Nae Afisa Ustawi wa Jamii Wilaya ya Bagamoyo, Bw. Rajab Mturuya akizungumza katika hafla hiyo ameelezea mafanikio ya kitengo cha Ustawi wa jamii Wilaya ya Bagamoyo katika kuhudumia Wazee amesema katika kipindi cha Mwaka 2018/2019 wamefanikiwa kutambua jumla ya Wazee 6113 katika Kata zote 11 za Halmashauri na hadi sasa jumla ya wazee 3416 wameshapatiwa vitambulisho vinavyowawezesha kupata huduma za Afya bure Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo na katika Vituo vingine vyote vya kutolea huduma za Afya vya Serikali katika Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo na kuanzisha mabaraza ya wazee katika Kata 07 kati ya 11ambazo ni Kata ya Mapinga, Kerege, Zinga, Kiromo, Makurunge, Nia njema na Yombo.

Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo imeadhimisha siku hii kwa Wataalam wa Afya kutoa huduma kwa Wazee katika Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo ambapo Wazee kwanza walipewa elimu na wataalam hao juu ya magonjwa yasiyoambukiza ambayo huwashambulia wazee kama vile, shinikizo la damu na utapiamlo unaosababishwa na lishe duni, mbali na magonjwa hayo Wazee hao walipewa elimu juu ya ugonjwa wa kifua kikuu, namna ya kujikinga na kuwahi matibabu wapatapo dalili za ugonjwa huo, umuhimu wa lishe bora na kupata mlo kamili wa kutosha kwa wakati na kwa usahihi, elimu juu ya Afya ya macho na umuhimu wa kufanya mazoezi ili kuboresha Afya zao.

Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo Rehema Kingu ambaye alimuwakilisha Mganga Mkuu Wilaya, akizungumza na Wazee, wataalam wa Afya na Wananchi waliojitokeza katika hafla hiyo amesema Idara ya Afya imefanikiwa kuanziasha madirisha maalum ya kuhudumia wazee kuanzia katika Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo na katika Vituo vyote vya kutolea huduma za Afya vya Serikali na madirisha hayo yanatoa huduma bure kwa wazee licha ya changamoto za upungufu wa dawa wanazopata lakini pia wanajitahidi kukabiliana nazo ili Wazee wapate huduma bora za Afya wakati wanapozihitaji.

Akifunga hafla hiyo, Bi. Rehema pia ametoa shukrani za dhati kwa wadau walioshirikiana nao katika kufanikisha hafla hiyo ambao ni taasisi ya Help Age na good Samaritan kwa kujitoa kwao hata kufanikisha hafla hiyo ambayo mbali ya kupatiwa huduma za Afya bure Wazee pia wamepewa huduma ya staftahi ya Asubuhi.


Matangazo

  • TANGAZO LA KUTEULIWA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 AWAMU YA PILI... May 09, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA BAGAMOYO... February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA OBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.. February 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI... July 14, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • HALMASHAURI YA BAGAMOYO YAPANDA MITI 500 ENEO LA MNADA WA ZINGA KUBORESHA MAZINGIRA...

    April 15, 2025
  • TUTAENDELEA KUSIMAMIA KWA DHATI NA HAKI MISINGI YA DEMOKRASIA...

    April 02, 2025
  • ELIMU KUHUSU MPOX YATOLEWA KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI...

    March 20, 2025
  • WAPENI ELIMU WANANCHI KUHUSU UGOJWA WA MPOX...

    March 17, 2025
  • Angalia zote

Video

SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 0733860575

    Simu ya kiganjani: 0733860575

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo