• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Divisheni na Vitengo
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TASAF
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Usimamizi wa Usafi na Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha mawasiliano Serikalini
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2024-2025
      • Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

LINDENI MISITU YA MIKOKO:WAZIRI UMMY

Posted on: February 17th, 2021

Hayo yamesemwa leo Februari 17, 2021 na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Muungano na Mazingira) Mhe Ummy Mwalimu kama maelekezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo kuhakikisha wanasimamia suala la Ulinzi wa misitu ya mikoko iliyopo pembezoni mwa Pwani ya Bahari ya Hindi Wilayani hapa.


Waziri Ummy Mwalimu amefanya ziara ya maalum ya kuangalia na kukagua uharibifu wa mazingira Wilayani Bagamoyo, ambapo ametembelea Kata ya Kiromo na kukagua athari za kimazingira katika machimbo ya mchanga na pia akatembelea Kata ya Zinga eneo la Pwani ya Kondo kuangalia utunzwaji wa maeneo ya Pwani kwa upandaji wa Miti ya Mikoko.


Mhe. Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Shirikianeni kwa karibu sana na Wakala wa misitu Nchini (TFS) kuhakikisha mnaongeza upandaji miti ya Mikoko katika Pwani ya Bahari ya Hindi na mhakikishe mnashirikiana na Wananchi katika Ulinzi wa Mikoko hii kwani Ulinzi wake ni jukumu la jamii nzima, ili kuimarisha utunzwaji wa mazingira ya Pwani ya bahari ya Hindi". Amesisitiza Mhe. Ummy


Akizungumzia faida za upandaji mikoko, Mhe Ummy ameongeza  kuwa miti hiyo inayopandwa pembezoni mwa bahari husaidia kulinda ardhi, kuhifadhi mazingira ya bahari, kulinda udongo katika bahari pia husaidia katika shughuli za kiuchumi kwa kutumika katika ufugaji wa nyuki hivyo kupata asali, na hata uvuvi wa samaki wadogo wadogo aina ya dagaa hivyo kusaidia kuongeza pato la Wananchi pamoja na Serikali.


Katika hatua nyingine Mhe. Ummy ameutaka uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo kuendelea kuwasimamia wafanyabiashara wanaochimba mchanga katika machimbo ya mchanga Kiromo, na kuhakikisha kuwa wachimbaji hao wanapo maliza shughuli za uchimbaji wanatunza na kuhifadhi mazingira ya eneo walilomaliza kufanya uchimbaji kwa kusawazisha eneo hilo na kupanda miti na kushauri uwekwe utaratibu wa  kuweka tozo maalum ya kuweka bond ili iwe rahisi kuwakamata wale watakaokimbia baada ya kumaliza shughuli ya uchimbaji na kuacha mashimo ambayo yanaleta athari baaadae lakini yanaacha uharibifu mkubwa wa mazingira.


Katika ziara hiyo Pia Mhe. Ummy amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo kwa kujitahidi kuthubutu kuonesha jitihada za uhifadhi wa taka ngumu kwa kutenga eneo la ukusanyaji wa taka yaani dampo jipya katika Kata ya Makurunge na kumshauri kufanya utaratibu wa kuanzisha vizimba vya kukusanyia taka za plastiki, chuma, na kuvitenga na vile vya uchafu wa kawaida kwani kwa njia hii taka Halmashauri inaweza kutengeneza fursa za ajira kwa Wananchi huku Uongozi wa Halmashauri ukiona pia namna ya kushawishi wafanyabiashara  wawekezaji  kuwekeza katika ukusanyaji wa taka kwani kwa njia hiyo inaweza kuibua fursa ya vijana kupata ajira pamoja na kutengeneza malighafi za viwanadani kama vile vifaa vya plastiki, vifungashio, mifuko ya salfeti na nk.


Mhe. Ummy amemalizia ziara yake hiyo kwa kushauri uboreshwaji wa kipengele katika utoaji wa Vibali vya ujenzi vinavyotolewa na Halmashauri kwa kuongeza kipengele cha kumtaka Mwananchi anayeomba kibali kuhakikisha anapanda miti sio chini ya minne katika kiwanja chake kabla au mara tu anapoanza ujenzi wa jengo lake kwani kwa kufanya hivi mazingira ya Mji wa Bagamoyo yataimarika.



Matangazo

  • TANGAZO LA KUTEULIWA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 AWAMU YA PILI... May 09, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA BAGAMOYO... February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA OBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.. February 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI... July 14, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • BAGAMOYO KUJITANGAZA KIMATAIFA SEKTA YA UTALIII...

    May 10, 2025
  • HALMASHAURI YA BAGAMOYO YAPANDA MITI 500 ENEO LA MNADA WA ZINGA KUBORESHA MAZINGIRA...

    April 15, 2025
  • TUTAENDELEA KUSIMAMIA KWA DHATI NA HAKI MISINGI YA DEMOKRASIA...

    April 02, 2025
  • ELIMU KUHUSU MPOX YATOLEWA KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI...

    March 20, 2025
  • Angalia zote

Video

SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 0733860575

    Simu ya kiganjani: 0733860575

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo