• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Divisheni na Vitengo
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TASAF
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Usimamizi wa Usafi na Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha mawasiliano Serikalini
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2024-2025
      • Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

WAZIRI WA ARDHI:ACHENI KUJIHUSISHA NA WIZI WA ARDHI.

Posted on: July 20th, 2021

Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.William Lukuvi amewaonya watu wote wanaojihusisha na wizi, ulanguzi wa ardhi kuwa wapo katika hatari ya kufunguliwa mashtaka na kupelekwa mahakamani ili kukomesha tabia hiyo ya unyang’anyi wa ardhi katika Halmashauri ya Wiaya ya Bagamoyo.

Ameyasema hayo wakati alipokuwa akizungumza na viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya Bagamoyo tarehe 20 Julai 2021 Mhe Lukuvi amesisitiza kuwa atawafunga watu wote ambao wanajiushisha na wizi pamoja na ulanguzi wa ardhi ‘’sitajali kuwa ni kiongozi wa serikali,kiongozi wa chama atakamatwa na atafunguliwa mashitaka na kupelekwa jela’’amesema Waziri wa Ardhi

Pia Mhe. Lukuvi amesema kuwa mpaka hivi sasa kwa upande wa Bagamoyo anaorodha ya matapeli 54 wakiwemo viongozi wa mitaa na kusema kuwa atawasoma hadharai ili wananchi wapate kuwafahamu na kusema kuwa ardhi ikifanyiwa vibaya inaweza kuhatarisha Amani hivyo haitowezekana kwa mtu kuibiwa ardhi yake huku viongozi wa sehemu husika wakiwepo.

Waziri wa Ardhi pia ametembelea eneo la Makurunge na kuzungumza na wananchi wa makurunge na kuwataka wananchi hao kuacha tabia ya kuvamia maeneo ambayo tayari serikali imewapatia wawekezaji huku wananchi hao wakitaka huruma ya serikali ili hali kuwa tayari wamekwisha fanya uvamizi katika maeneo ambayo sio ya kwao.

‘’wananchi muache tabia ya kufanya uvamizi wa katika maeneo yaliyo tolewa na serikali kwa ajili ya uwekezaji kwani kufanya hivyo ni kinyume na taratibu’’amesema Mhe.Lukuvi.

Aidha Mhe. Waziri amemtaka mwekezaji kampuni ya Genenter na Green Wuud  anaemiliki ekari  Zaidi ya 1000 na kushindwa kuliendeleza kwa muda mrefu na kusababisha wananchi kuvamia na kuibua mgogoro kupeleka mpango kazi wa uendelezaji wa shamba hilo kwani kuna malalamiko mengi ambayo yanatokana na uwepo wa shamba hilo ambalo halijaendelezwa kwa muda mrefu

‘’kufikia tarehe 22 saa saba mchana wamiliki wote wa haya maeneo wafike ofisi kwangu kwa ajili mazungumo na waziri pia mwekezaji wa kampuni ya Genenter na Green Wuud   kuwasilisha mpango kazi wa uendelezaji wa shamba hilo ili tuweze kuondoa mgogoro huu baina yako na wananchi wa hapa’’amesema Mhe. Lukuvi.

Waziri Lukuvi pia ameweka wazi kuwa eneo la lazaba ni mali ya serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar tangu awamu ya kwana ya Mwalimu Nyerere na kuwataka wananchi wote ambao wanaishi katika eneo hilo kundoka mara moja kwani wao ni wavamizi katika eneo hilo.

‘’leo nataka niseme tangu awau ya kwanza Mwalimu Nyerere alitoa shamba la lazaba kwa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar lile shamba bado ni la Zanzibar yeyote anaekwenda kule ni mvamizi mimi ninayo mikataba tangu awamu ya kwanza mapaka leo na nitasimamia hiyo mikataba kuhakikisha lile shamba waliopewa Serikali ya Mapinduzi ya Zazniabar  linabaki kuwa la Salama’’amesema Waziri.

Sanjari na hayo Waziri wa Ardhi ameamuru kukamatwa kwa  watu watano akiwemo katibu Mwenezi wa chama cha Mapinduzi (CCM)Kata ya Mapinga Omar Shaaban na kuliagiza jeshi la polisi kuwafanyia mahojiano kwa tuhuma za kuhusika na utapeli wa kuuza ardhi za wananchi kiholela na kusababisha migogoro mingi katika kata hiyo.

Nae mkuu wa mkoa wa Pwani ABOUBAKA kunenge  alieleza kukithiri kwa migogoro ya ardhi ndani ya mkoa wake huku baadhi ya viongozi wa kata ya mapinga wakieleza ushiriki wa baadhi ya viongozi wenzao wa CCM kuuza na kuchochea migogoro ya ardhi Mapinga..  

Ziara hii ya Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.William Lukuvi  ni operesheni yake endelevu ya ondoa Migogoro ya ardhi mkoani Pwani..

Matangazo

  • TANGAZO LA KUTEULIWA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 AWAMU YA PILI... May 09, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA BAGAMOYO... February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA OBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.. February 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI... July 14, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • HALMASHAURI YA BAGAMOYO YAPANDA MITI 500 ENEO LA MNADA WA ZINGA KUBORESHA MAZINGIRA...

    April 15, 2025
  • TUTAENDELEA KUSIMAMIA KWA DHATI NA HAKI MISINGI YA DEMOKRASIA...

    April 02, 2025
  • ELIMU KUHUSU MPOX YATOLEWA KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI...

    March 20, 2025
  • WAPENI ELIMU WANANCHI KUHUSU UGOJWA WA MPOX...

    March 17, 2025
  • Angalia zote

Video

SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 0733860575

    Simu ya kiganjani: 0733860575

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo