• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Divisheni na Vitengo
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TASAF
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Usimamizi wa Usafi na Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha mawasiliano Serikalini
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2024-2025
      • Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

Kitengo cha TASAF

Mratibu wa TASAF katika Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo ni Ndg. Jalala Sammatta.

Simu: +255 784 422 554


UTANGULIZI

Wilaya ya Bagamoyo ni moja kati ya Wilaya saba zilizopo katika Mkoa wa Pwani. Wilaya ina Halmashauri 2 ambazo ni halmashauri ya Wilaya Bagamoyo na Halmashauri ya Chalinze. Kulingana na takwimu za mwaka 2012 Wilaya ya Bagamoyo ilikuwa na idadi ya jumla ya wakazi 311,740, wanaume 154,198 na wanawake 157,542. Kiutawala Wilaya ya Bagamoyo ina Tarafa 7, kata 26 Vijiji 76 na vitongoji 611. Mpango wa kunusuru kaya maskini una tekeleza katika kata zote 26 na katika vijiji 66. Jumla ya kaya 12,085 zenye idadi ya walengwa 48,340 (me 16,113, ke 32,227) zilitambuliwa wakati wa kuanza kwa mpango. Jumla ya kaya za walengwa zimepungua hadi kufikia 10,508 kwa sasa kutokana na sababu mbalimbali likiwemo zoezi la uhakiki. Kaya zilizoodolewa wakati wa uhakiki zilikuwa 987.

Wilaya ya Bagamoyo ni miongoni mwa Wilaya zinazotekeleza Mpango wa TASAF awamu ya tatu wa kunusuru kaya maskini kutoka Octoba, 2013. Utekelezaji wa mpango katika Halmashauri ya Bagamoyo umefanikiwa kutekelezwa katika sehemu nne za mpango ambazo ni Mpango wa uhawilishaji fedha( Cash Transfer), Mpango wa ajira za muda (Public Work Projects), Mpango wa ujenzi wa miundombinu maeneo yasiyokuwa nazo (Targeted Infrastructure) na Mpango wa kuweka akiba na kuwekeza (Livelihood Enhacement).

1.MPANGO WA UHAWILISHAJI FEDHA

Katika mpango wa Uhawilishaji fedha, ruzuku imeendelea kutolewa kwa kaya za walengwa 10,508 ambapo jumla ya Tshs 8,855,241,152.00 zimetolewa kwa awamu 22 mfululizo toka Januari-Februari 2014 hadi kufika Julai-Agositi 2017. Ruzuku kwa kaya masikini hutolewa ili kuiwezesha kaya kumudu mahitaji muhimu ambayo ni chakula, afya na elimu.

Jumla ya wanafunzi wa shule ya msingi 4,542 (me=2147, ke. 2395) na wanafunzi wa shule za sekondari 620 (me 303 ke 317) wanaendelea na masomo kutokana na kupata mahitaji ya shule.

2.PROGRAM YA MIRADI YA AJIRA YA MUDA KWA KAYA MASKINI (PWP)

Wilaya ya Bagamoyo ilianza kutekeleza mpango wa kutoa ajira za muda kwa kaya za walengwa kuanzia mwaka 2014/2015. Katika mpango huu Jamii huibua miradi na miradi hiyo hutekelezwa na kaya masikini zilitambuliwa katika kijiji husika.

Lengo la miradi hii ni kupunguza umasikini wa kipato kwa jamii husika kwa kaya kupata ruzuku baada ya kushiriki kutoa nguvu kazi kipindi cha hari kwa kutekeleza miradi iliyoibuliwa katika kijiji, ambapo kaya inapaswa kushiriki siku 15 kwa mwezi na kwa miezi mine kwa kulipwa shilingi 2,300 kwa siku, hivyo kaya ikishiriki siku zote 15 inapata 34,500.00 kwa mwezi na 138,000.00 kwa miezi minne

Kwa kipindi cha utekelezaji mwaka 2014 / 2015, Tshs 1,292,761,000/- zililipwa kwa kaya za walengwa 10,363 9 (Me 1,749, Ke 8,614), Miradi 141 iliibuliwa na kutekelezwa kama ifuatavyo:-

1.Vitalu vya miti - 4

2.Ukarabati wa viwanja vya mpira - 3

3.Utengenezaji wa njia za kuzuia moto - 1

4.uchimbaji wa visima - 1

5. kuhifadhi vyanzo vya maji - 1

6.ukarabati wa barabara za jamii - 123

7.kutengeneza njia za waenda kwa miguu na ujenzi wa vivuko vya waenda kwa miguu – 2

8.Ukarabati wa mabwawa – 6

UTEKELEZAJI WA PROGRAMU YA MIRADI YA AJIRA ZA MUDA KWA MWAKA WA 2016/2017.

i) MAFUNZO KWA WATAALAMU ELEKEZI, WANAKAMATI, WATENDAJI WA VIJIJI NA WENYEVITI WA VIJIJI.

utekelezaji wa miradi ya ajira za muda ulianza kwa kutoa mafunzo elekezi kwa wawezeshaji 33 wa ngazi ya wilaya, wawezeshaji hao walienda katika vijiji na kushirikiana na serikali za vijiji kuchagua wataalamu elekekezi ngazi ya jamii.

Aidha mafunzo ya usimamizi na utekelezaji wa miradi, taratibu za manunuzi, upangaji wa kazi wa kila siku yalitolewa kwenye vijiji vyote vinavyotekelezaji mpango ambapo jumla ya wenyeviti wa vijiji 66, watendaji 66,watalam washauri 66,wawakiishi wa serikali ya vijiji 66 na wanakamati 264.

ii)UTEKELEZAJI WA MIRADI YA AJIRA ZA MUDA 2016 / 2017

Utekelezaji wa miradi ulianza mwezi Januari na kukamilika mwezi April, 2017.

Jumla ya miradi 99 iliibuliwa kufanyiwa usanifu na kutekelezwa katika vijiji 66 vinavyotekeleza Mpango, Miradi iliibuliwa na jamii kwa kushirikisha makundi yote katika jamii. Jamii iliweza kutambua changamoto zinazowakabili, kutambua fursa zilizopo na kuweka vipaumbele na hatimaye kuibua miradi yao.

Miradi iliyoibuliwa, kusanifiwa na kutekelezwa ni kama inavyoonekana katika jedwali. Walengwa 9,266 wameshiriki katika kazi za ajira ya muda na kulipwa jumla ya fedha za kitanzania 1,215,064,700.00

Na.Aina ya mradiIdadi ya miradi

1Upandaji wa miti 43

2Ukarabati na ujenzi wa malambo na visima 48

3Hifadhi ya udongo, makinga maji na kusafisha mifereji ya maji ya mvua 8

JUMLA99

iii)MAFANIKIO

1.Kaya za walengwa 9,266 zimeweza kushiriki katika kutekeleza miradi na kulipwa ujira fedha za kitanzania 1,215,064,700.00 hivyo kumudu kununua mahitaji ya msingi katika kipindi cha hari.

2.Upatikanaji wa miundombinu ya uvunaji wa maji ya mvua mfano malambo na visima.

3.Miti ya matunda, mbao na kivuli iliyopandwa inatazamiwa kuboresha lishe na mazingira katika maeneo yao.

4.Walengwa wameweza kupata ujuzi wa upandaji miti, uhifadhi wa udongo na technilogia za uvunaji maji mfano makinga maji na utengenezaji malambo.

5.Walengwa wameanza kuweka akiba kutokana na fedha za uhawilishaji na ajira ya muda kwa lengo kuwekeza katika miradi ili kuongeza kipato.

3.MPANGO WA KUWEKA AKIBA NA KUWEKEZA (LIVELIHOOD ENHACEMENT).

Mpango unalenga kuziunganisha kaya za walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya maskini kujiunga pamoja katika vikundi vya kaya kuanzia kaya 10 -15 na kuanzish vikundi vya kuweka akiba na kuwekeza.

Vikundi 449 vyenye idadi ya kaya 6,045 (me 913, Ke 5240) vimeundwa kwa hiari katika vijiji vyote 66 vinavyotekeleza Mpango wa kunusuru kaya maskini. Vikundi hivi vimepata masanduku ya chuma, mafunzo ya uundaji wa vikundi, kuandaa katiba na vinaendelea kupewa mafunzo na maafisa ugani ya namna ya kuanzisha miradi midogo midogo ya kuongeza kipato mfano kulima bustani, magenge, ufugaji, kilimo na pindi wakipata fedha za uhawilishaji na ajira ya muda waweze kuweka akiba lengo likiwa ni kutoka katika umaskini. Aidha vijana 200 wenye umri wa miaka kati ya 18 hadi 35 kutoka katika kaya za walengwa wamepatiwa mafunzo ya stadi za ujasiriamali. Mafunzo hayo yamefanyika kuanzia tarehe 21 – 27 Agositi, 2017 ambapo kila kijana aliibua mradi wa chagua lake na waliahidi kuanza utekelezaji wake mara moja. Vituo vya mafunzo na vijiji vilivyotoa vijan walioshiriki mafunzo ni kama inavyoonekana katika jedwali. Kila kituo kilikuwa na vijana 50 na mafunzo haya yalitolewa kwa ushirikiano na mamlaka ya utekelezaji Bagamoyo, TASAF makao makuu na Benki ya Dunia.

Na.KituoVijiji

1. ZingaZinga, Kondo, Kerege, Mapinga.

2. DundaDunda , Kaole

3. KiwangwaKiwangwa, Bago, Mwetemo, Masuguru

4. LugobaMindutulieni, Makombe, Kinzagu, Saleni, Mindukene

Aidha kuanzia tarehe 11 – 16 Septemba Mafunzo ya kuweka akiba na kuwekeza yatatolewa kwa walengwa wa vijiji vitatu vya Mwavi, Mwetemo na Masuguru. Mafunzo haya yameendelezwa na kufanyiwa majaribio katika kijiji cha Kiharaka na kuonekana kuwa na manufaa kwa mazingira ya watu wa Bagamoyo. Tunatalajia kuendelea kutoa mafunzo haya kwa vijiji vyote vya mpango kadiri bajeti itakavyorusu.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUTEULIWA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 AWAMU YA PILI... May 09, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA BAGAMOYO... February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA OBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.. February 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI... July 14, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • BAGAMOYO KUJITANGAZA KIMATAIFA SEKTA YA UTALIII...

    May 10, 2025
  • HALMASHAURI YA BAGAMOYO YAPANDA MITI 500 ENEO LA MNADA WA ZINGA KUBORESHA MAZINGIRA...

    April 15, 2025
  • TUTAENDELEA KUSIMAMIA KWA DHATI NA HAKI MISINGI YA DEMOKRASIA...

    April 02, 2025
  • ELIMU KUHUSU MPOX YATOLEWA KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI...

    March 20, 2025
  • Angalia zote

Video

SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 0733860575

    Simu ya kiganjani: 0733860575

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo