• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
    • Baraza la Madiwani
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
      • Baraza la Madiwani
        • Historia
        • Dhima na Dira
        • Muundo wa Taasisi
        • UKARIBISHO
        • service one
        • what we do
        • Utalii
        • Kaole Snake Park
        • Kaole Mamba Ranch
        • Completed
        • Elimu
        • Afya
        • Maji
        • Caravan Serai
        • Education
        • Ukaguzi wa Ndani
        • TAARIFA YA O& OD
        • Miradi iliyopendekezwa
        • Bajeti ya Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo
        • Maendeleo ya Jamii
        • Elimu Msingi
        • Elimu Sekondari
        • Ujenzi
        • Mfuko wa Jamii
        • Mifugo na Uvuvi
        • Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
        • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
        • Idara ya Maji
        • Sheria ndogo za Halmashauri
        • Ardhi na Mipango Miji
        • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
        • Sheria
        • Ufugaji Nyuki
        • Usafishaji na Mazingira
        • Fedha na Biashara
        • Election Unit
        • Ugavi na Manunuzi
        • Maeneo ya Uwekezaji
        • TEHAMA na Uhusiano
        • Kupata Fomu Mbalimbali
        • Madiwani
        • Baraza la Madiwani
        • Orodha ya Wahe.Madiwani
        • Kamati za kudumu za Halmashauri
          • Elimu, Afya na Maji
          • Fedha, Uogozi na Mipango
          • Kamati ya UKIMWI
          • Kamati ya Maadili
          • Uchumi, Ujenzi, Mipango miji na Mazingira
        • Ratiba za Vikao vya Kisheria
        • Ratiba
          • Kuonana na Mhe. Mwenyekiti
          • Ratiba ya Vikao vya Wahe. Madiwani
        • Mpango Mkakati
        • Bajeti ya Halmashauri
        • Mkataba wa huduma kwa Mteja
        • ZABUNI MBALI MBALI ZA UWAKALA
    • Baraza la Madiwani
  • Idara na Vitengo
    • Mifugo na Uvuvi
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Elimu Sekondari
      • Works
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Usafi na Mazingira
      • Fedha na Biashara
      • Maji
      • Elimu Msingi
    • Kitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Election Unit
      • TEHAMA na Uhusiano
  • Huduma
    • Elimu
    • Afya
    • Maji
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2018/2019
    • Mkataba wa huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MPYA
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

Maendeleo ya Jamii


IDARA YA MAENDELEO YA JAMII NA USTAWI WA JAMII

Idara ya Maendeleo ya Jamii na ustawi wa Jamii ni miongoni mwa Idara 13 katika Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo.


WATUMISHI

Hadi mwezi Juni, 2017, Idara ilikuwa na jumla ya watumishi 31 kati yao wanawake ni 23 na wanaume 7. Aidha kati ya watumishi hao, watumishi walioko Maendeleo ya jamii ni 24 na 7 ni watumishi wa Ustawi wa jamii.

 Idara ya Maendeleo ya Jamii na ustawi wa Jamii inaundwa na vitengo vifuatavyo: -

(i)Utafiti, mipango na Takwimu

(ii) Jinsia watoto.

 iii) Vijana

 (iv)  Ufundi na ujenzi

(iv) Dawati la Uwezeshaji wa wananchi kiuchumi.

v) Mpango wa Kudhibiti UKIMWI  

(vi) Ustawi wa Jamii.


MAJUKUMU YA IDARA YA MAENDELEO YA JAMII NA USTAWI WA JAMII.


i)Kuwezesha jamii kupanga na kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo    vijijini kwa kuzingatia masuala ya kijinsia.


ii)Kuraghibisha jamii katika kubuni, kupanga, kutekeleza na kutathmini miradi yao ya maendeleo kupitia mpango wa O&OD.


iii)Kuhamasisha jamii kuondokana na mila potofu na kuwa na mtazamo wa kupenda mabadiliko.


iv)Kuhamasisha jamiii katika matumizi ya teknolojia rahihi na sahihi katika kuleta maendeleo.


i)Kuelimisha jamii kuhusu haki za mtoto.


i)Kuratibu uanzishaji, kufuatilia utendaji na kutoa ushauri wa kitaalam kwa mashirikia yasiyo ya kiserikali (NGOs) yanayojihusisha na kuchangia maendeleo katika Halmashauri.

ii)Kuhamasisha jamii kuunda vikundi mbali mbali vya kijamii (CBOs) jamii ili kujiajiri na kuongeza kipato na kuratibu masuala ya utoaji wa mikopo kwa vikundi vya wanawake na vijana.

ii) Kusimamia utekelezaji wa Sera mbali mbali za maendeleo ikiwa ni pamoja na Sera zinazohusu masuala ya Maendeleo ya Jamii.

iii)Kuwezesha Halmashauri na Vijiji kuingiza masuala ya jinsia katika mipango na bajeti yao.

iv)Kusaidia kamati za maendeleo za vitongoji, vijiji na Kata kuingiza masuala mtambuka katika kupanga shughuli zao maendeleo.

v) Kushirikiana na Asasi zisizo za kiserikali katika kusaidia jitihada za jamii katika utekelezaji wa miradi yao ya maendeleo.

 vi) Kutoa huduma za Ustawi wa Jamii kuhusiana na masuala ya watoto, na huduma kwa wazee na walemavu.


2. MGAWANYO WA MAJUKUMU KWA KILA KITENGO: -

 (I) KITENGO CHA UTAFITI, MIPANGO NA TAKWIMU

Kuunganisha takwimu zote za maendeleo zinazowasilishwa kutoka kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii ngazi ya kata ili kutambua mahitaji halisi ya jamii na kutumia takwimu hizo katika kuandaa mipango mbali mbali ya maendeleo.

Kuratibu mpango kazi wa Idara, mpango wa manununzi na cash flow.

Kusimamia maandalizi ya taarifa mbalimbali za Idara

Kuratibu maandalizi ya bajeti, taarifa na uhamasishaji

Kufanya ufuatiliaji na kuunganisha (compile) taarifa za utendaji za kila robo kutoka kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii ngazi ya kata ili kuwa sehemu ya taarifa ya Idara kwa kipindi husika.

(II) KITENGO CHA JINSIA NA WATOTO


Huratibu na kufuatilia masuala yatakayowezesha kuwepo kwa usawa wa haki za kijinsia katika jamii.

Huratibu na kusimamia sera ya maendeleo ya wanawake na jinsia katika sehemu zote ndani ya Idara na nje ya Idara.

Huratibu na kuhamasisha uanzishwaji na uendeshaji wa Vikundi vya kiuchumi kama SACCOS, MITANDAO na VICOBA

Kupata taarifa ya uhai wa vikundi vya wanawake vya kiuchumi.

Kupata vikundi hai vya wanawake vyenye miradi halisi ambavyo vitawezeshwa kwa kupatiwa mkopo kupitia mfuko wa wanawake Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo.

Kufanya ufuatiliaji wa fedha za Wizara ya Maendeleo Jamii kwa ajili ya kukopesha vikundi/ Mitandao, VICCOBA na SACCOS za wanawake waliokidhi vigezo.

Kufanya ufuatiliaji wa marejesho kwa vikundi vya wanawake vinavyokopeshwa kupitia mfuko wa wanawake.

Kutoa mafunzo ya ujasiriamali na uendeshaji wa miradi ya vikundi vya wanawake.

Kuhakikisha masuala ya kijinsia yanaingizwa katika mipango ya Halmashauri.

Kuanisha masuala ya kijinsia kwa ajili ya kushughulikia.

Kutoa maelekezo na utaratibu kwa vikundi juu ya utaratbu wa kuvitambua na hadi kupatiwa vyeti.

(III) KITENGO CHA VIJANA

Kuratibu shughuli za Vijana sambamba na kusimamia sera ya vijana


Kuratibu na kuhamasisha uanzishwaji na uendeshaji wa Vikundi vya

kiuchumi kama SACCOS na VICOBA


Kuhakiki vikundi vya vijana kwa ajili ya: -


•Kupata taarifa ya uhai wa vikundi vya vijana vya kiuchumi

•Kupata vikundi hai vya vijana vyenye miradi halisi ambavyo vitawezehwa kwa kupatiwa mkopo kupitia mfuko wa vijana Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo.

•Kusaidia kuandika maandiko mradi kwa vikundi vya vijana yakuomba fedha Wizarani.

•Kufanya ufuatiliaji wa marejesho kwa vikundi vya vijana vilivyokopeshwa kupitia mfuko wa vijana.

•Kutoa mafunzo ya uanzishaji na uendeshaji wa vikundi vya vijana na ya ujasiriamali.


 (IV) KITENGO CHA UFUNDI NA UJENZI


Kutoa ushauri wa kiufundi kwa mafundi wa vijiji katika ujenzi wa miradi ya kujitolea vijijini inayohusu kazi za kiufundi kama ujenzi wa madarasa, zahanati, nyumba za walimu nk.

Kuanzisha na kuhamasisha vikosi vya kiufundi vijijini kwa lengo la kutumia vikosi hivyo kwa shughuli mbali mbali za maendeleo vijijini.

Kusaidia mafundi na wananchi vijijini kuandaa makadirio ya gharama na vya miradi ya ujenzi.

Kuratibu mafunzo ya ufundi kwa vijana.

Kuainisha teknolojia sahihi kwa shughuli za ufundi vijijini.

Kuandaa na kuwasilisha taarifa za utekelezaji wa kazi ya kikosi cha ufundi kwa vipindi vya robo mwaka kwa Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri.

Kufanya kazi nyingine utakazopangiwa na mkuu wa Idara/Mkurugenzi wa Halmashauri


(V) DAWATI LA UWEZESHAJI WA WANANCHI KIUCHUMI


Kuratibu shughuli za uwezeshaji Wananchi Kiuchumi katika Halmashauri ya Wilaya.

Kusimamia na kufuatilia shughuli za uwezeshaji zinazofanywa katika Kata na Vijiji.

Kutafsri na kusimamia utekelezaji wa Sera na Sheria ya Taifa ya uwezeshaji Wananchi.

Kukusanya taarifa na tafiti mbalimbali na kumshauri Mkurugenzi Mtendaji wa H/W katika masuala ya uwezeshaji.

Kuhamasisha uundwaji na usajili wa vikundi vya kijamii na kufanya uzalishaji wenye tija.

Kuhakikisha fedha za uendeshaji zinatengwa katika bajeti kila mwaka ili;

•Kuratibu na kuhamasisha uanzishwaji na uendeshaji wa Vikundi vya kiuchumi kama SACCOS na VICOBA.

•Kuwasilisha taarifa ya utekelezaji kwa Kamati ya uwezeshaji ya Halmashauri na kuituma kwa Mratibu wa Uwezeshaji wa Mkoa na kunakiliwa Baraza la Taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi (NEEC).

•Kuratibu shughuli za mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs).


 (IV) MPANGO WA KUDHIBITI UKIMWI


Kutambua vichocheo vya maambukizi ya VVU katika Wilaya, kata, vijiji/vitongoji na kuweka mkakati wa kudhibiti Ukimwi.

Kushirikiana na wadau wa mapambano dhidi ya Ukimwi katika kutekeleza afua za Ukimwi.

Kutathmini hali halisi ya Ukimwi katika Wilaya.

Kutambua na kutathmini shughuli za wadau mbali mbali katika masuala ya Ukimwi katika Wilaya.

Kuratibu mipango ya VVU na Ukimwi kutoka ngazi ya Kata, Vijiji na mitaa.

Kutoa ushauri kwa ngazi za Kata, Vijiji na Vitongoji kuhusu sera au sheria ndogo juu ya udhibiti wa Ukimwi.

Kuhakikisha kamati za kudhibii Ukimwi zinaundwa na kufanya kazi kwa kufuata utaratibu, miongozo na sheria zilizopo.

Kupokea na kujadili taarifa za utekelezaji wa shughuli za kamati za kudhibiti Ukimwi za kata, mitaa na vijiji.

Kutoa taarifa ya shughuli za VVU na Ukimwi kwa kamati ya Ukimwi ya Wilaya (CMAC) na kamati za kudumu za Halmashauri    kila robo mwaka.

Kuhakikisha uwepo wa orodha ya wadau wanaoshughulika na afua za VVU na UKIMWI katika Wilaya.

Kuhakikisha uwepo wa takwimu za WAVIU na watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi.

 

(VI) KITENGO CHA USTAWI WA JAMII.


Kitengo cha Ustawi wa Jamiii kina vitengo vidogo vitatu vilivyo na majukumu yafuatayo: -

i) Kitengo cha huduma ya ustawi wa jamii familia na watoto; malezi makuzi na maendeleo ya watoto wadogo.

Kitengo hiki kinatoa huduma zake kwa kuzingatia Sera, Miongozo, Kanuni na sheria zifuatazo;

i.i.     Sheria ya Ndoa Na.5 ya mwaka 1971.


i.ii.     Sheria ya mtoto Na. 21 ya mwaka 2009.


i.iii.  Sheria ya kuzuia Usafirishaji Haramu wa Binadamu “The Anti Traficking in Persons Act 2008.


Huduma zinazotelewa ni pamoja na;

i)Huduma za usuluhishi wa ndoa zenye mifarakano

Kufanya unasihi kwa wanandoa na mifarakano ili kupata suluhu ya matatizo yanayowakabili na kuwawezesha kuishi kwa Amani na upendo.

Kusimamia makubaliano yaliyofikiwa na wanandoa katika usuluhishi ili kuimarisha mahusiano baina yao na watoto wao.

Kutoa mafunzo kwa wanandoa, familia kabla au baada ya ndoa kwa lengo la kuwapa stadi au kuboresha mahusiano kupitia stadi za mawasiliano (Communication Skills), maamuzi (Decision Making), utatuzi wa matatizo (Conflict Resolution skills) na Stadi za malezi (Effective Parenting and Care taking skills).

Kuelekeza mashauri ya ndoa katika mahakama pale usuluhishi unapokuwa umeshindikana.

Kujenga uwezo wa unasihi, usuluhishi na upatanishi (Counseling, reconciliation and mediation) kwa mabaraza ya usuluhishi wa ndoa ya kata na yale ya madhebu ya dini.


ii) Huduma za matunzo kwa watoto walio katika ndoa zilizo katika mifarakano.

Huduma hii hutolewa ili watoto waliozaliwa kwenye ndoa zenye mifarakano waweze kupata haki na huduma wanazostahili kazi zinazofanyika ni pamoja na;

Kufanya uchunguzi wa kijamii kupata taarifa sahihi ili kupata taarifa sahihi kuhusu tatizo

Kufanya unasihi na wanandoa na familia ili wafikie makubaliano namna ya kuwatunza watoto na kusimamia utekelezaji wa makubaliano hayo

Kuelekeza mashauri mahakamani kwa uamuzi wa kisheria endapo makubaliano ya hiari hayakufikiwa


iii)Huduma na matunzo ya watoto waliozaliwa nje ya ndoa.


Huduma hii hutolewa ili watoto waliozaliwa nje ya ndoa waweze kupata haki na huduma wanazostahili kazi zinazofanyika ni pamoja na;

Kufanya uchunguzi wa kijamii kuhusu malalamiko kutoka kwa akina mama wajawazito au watoto waliozaliwa nje ya ndoa na ambao baba zao hahawajibiki kuwatunza.


Kufanya unasihi kwa wahusika ili waweze kufikia makubaliano ya hiari kuhusu matunzo na malezi ya watoto husika na kusimamia makubaliano yaliyofikiwa.


Kufanya upatanishi ili kuondoa mvutano baina ya wazazi ili kuepeusha athari za kisaikolojia kwa watoto.


Kuelekeza mashauri mahakamani kwa uamuzi wa kisheria endapo makubaliano ya hiari hayakufikiwa.


iv)Huduma ya Makao ya kulelea watoto yatima na walio katika mazingira hatarishi.


Huduma ya malezi matunzo na ulinzi kwa watoto yatima na walio katika mazingira hatarishi inatolewa kwa watoto ambao wamekosa wazazi, ndugu na jamaa wa kuwalea na kutokana na sababu mbalimbali. Serikali, mtu binafsi, na mashirika ya hiari, mashirika yasiyokuwa ya kiserikali yanaweza kuanzisha na kuendesha makao ya watoto yatima. Anaeanzisha na kuendesha makao ya watoto yatima lazima awe na uwezo wa kutekeleza mambo yote kwa mujibu wa maelekezo yaliyotolewa na sheria na muongozo wa uanzishaji na uendeshaji wa makao hayo kazi zinazofanyika ni pamoja na:

Kufanya ukaguzi wa eneo linalokusudiwa kwa shughuli hiyo


Kutoa leseni ya umiliki na uendeshaji kwa muombaji aliyekidhi masharti na vigezo vya kutoa huduma hiyo


Kusimamia na kuratibu huduma zinazotolewa kwa watoto makaoni.


Kutoa idhini kwa mtoto anayetunzwa katika makao kuchukuliwa na mlezi/walezi wa kambo.


Kupokea na kuchambua taarifa mbalimbali za utekelezaji na mapato na matumizi kutoka kwa viongozi wa makao 10 11.


Kufanya ukaguzi katika makao na kutoa ushauri wa kitaalamu kila inapohitajika.


Kufanya uchunguzi wa kijamii ili kujua sababu zinazofanya mtoto/watoto kuwa na hitaji la malezi katika makao.


 Kufanya ufuatiliaji nyumbani kwa walezi, ndugu na wazazi ili kuwaandaa kupokea mtoto/watoto wanaolelewa kwenye makao.


Kuwatengamanisha wanaokulia makaoni ili waweze kujumuika na kujitegemea kwenye jamii.


Kutoa mafunzo ya malezi na ulinzi wa watoto kwa viongozi na walezi wa watoto yatima na walio katika mazingira hatarishi.


 Kuelimisha jamii kuhusu athari za malezi ya watoto katika makao.


 Kuhamasisha Jamii kuhusu taratibu za uanzishaji na uendeshaji wa makao ya kulea watoto wenye shida.


v)Huduma ya malezi ya kambo na kuasili

Huduma hii hutolewa kwa watoto ambao wamekosa malezi, matunzo na ulinzi toka kwa wazazi/walezi na ndugu kutokana na sababu mbalimbali kama vile kifo, kutelekezwa. Kazi zinazofanyika ni pamoja na;


Kufanya uchunguzi wa kijamii kwa watu wanaoomba watoto kwa ajili ya malezi ya kambo


Kufanya uchunguzi wa kijamii kwa watoto wanaostahili kupewa kibali cha malezi ya kambo


Kufanya mawasiliano na International Social Services kwa lengo la kupata maoni na mapendekezo kutoka nchi za nje kuhusu waombaji ambao sio raia wa Tanzania.


Kutoa kibali cha malezi ya kambo kwa waombaji walioidhinishwa na Kamishna wa Ustawi wa Jamii.


Kufanya ufuatiliaji wa malezi, makuzi na maendeleo ya watoto alio katika malezi ya kambo.


Kutoa ushauri kwa walezi wa kambo kuchukua hatua za kuasili watoto baada ya kutimiza kipindi cha miezi mitatu cha malezi ya kambo na kuridhika na malezi yao.


Kuandaa na kuwasilisha taarifa ya kijamii Mahakama Kuu ya Tanzania kuhusu maombi ya kuasili mtoto.


 Kuelimisha jamii kuhusu huduma na taratibu za malezi ya kambo na kuasili.


vi). Kitengo cha marekebisho ya tabia na haki za mtoto kisheria:

Kitengo hiki kinatoa huduma kwa kuzingatia Sera, Miongozo, Kanuni na Sheria mbalimbali. Sheria hizo ni;


I.Sheria ya mtoto ya mwaka 2009


II. Sheria ya Huduma za Majaribio na Ujenzi wa Tabia (Sura Na.247)


III. Sheria ya Makosa ya Kujamiiana Na.4 ya Mwaka 1998


IV.Sheria ya Kanuni za adhabu (Sura ya 16)


V.Sheria ya Huduma kwa jamii Na.6 ya Mwaka 2002


Huduma zinazotolewa ni pamoja na: -


i) Haki za watoto/vijana (Juvenile Justice)

Mtoto au kijana anayeshitakiwa kwa kosa la jinai anapaswa kupelekwa katika mahakama ya watoto (Juvenile Court) au ambayo mazingira yake yanalingana nayo.

Aidha watoto/vjijana wanapaswa kupelekwa katika mahabusi za watoto (Retention Homes) badala ya mahabusi za wakubwa (Remand Prison), pale ambapo wamekosa dhamana au kosa lake halistahili dhamana.

 Iwapo wanapatikana na hati kwa kosa la jina na iwapo umri wao ni chini ya miaka 16 Afisaustawi wa Jamii atawasilisha taarifa mahakamani.

Taarifa hii itamwezesha hakimu kupata picha kamili kuhusu maisha na mazingira ya mshitakiwa kabla ya kutoa hukumu.

Taarifa hii pia itasaidia hakimu kutoa hukumu ya kumpeleka mtoto chini ya usimamizi na uangalizi wa Afisa ustawi wa Jamii kwa muda usiopungua miezi 12 na usiozidi miezi 36, au atahukumiwa kwenda katika shule ya maadhimisho (Approved School) kwa muda kati ya miezi 12 na 36 badala ya kuhukumiwa kwenda kutumikia kifungo chake katika jela ya watu wazima.

Huduma zitolewazo katika Mahakama ya watoto ni;

Kuunganisha huduma za Ustawi wa Jamii na Sheria za watoto katika mahakama na wadau mbalimbali kama Mahakimu, Wanasheria, Polisi, Jumuiya za wananchi, Mashirika yasiyo ya Ki-Serikali na Mashirika ya Kidini.


Kufanya mahojiano na mtoto/kijana mshitakiwa ili kupata chanzo na sababu ya tatizo.


Kuiwasilisha taarifa hiyo Mahakakamani ili kumsaidia Hakimu kutoa maamuzi kwa maslahi ya mtoto/kijana (Social Enqirery Report).


Kuweka mkataba wa marekebisho ya tabia na mteja.


Kusimamia na kufuatilia mwenendo na tabia za mtoto/kijana.


Kuwaunganisha watoto/vijana na wazazi/walezi.


Kuunganisha mipango ya uwezeshaji haki jamii na mipango ya kitaifa kama vile MKUKUTA, MKURABITA, Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, na Malengo ya Milenia (MDGs).


 Kupanga na kutekeleza mikakati ya mawasiliano na ushirikiano wa Wizara mbalimbali pamoja na Taasisi nyingine zinazojishughulisha na Haki za Jamii.


Kuhakikisha kwamba mipango yote inaendeshwa katika viwango vya Ubora

vii). Kitengo cha huduma kwa watu wenye ulemavu na wazee:

Kitengo hiki kinatoa huduma kwa kuzingatia Sera, Miongozo, Kanuni na Sheria zifuatazo

Sera

I.Sera ya Taifa ya Wazee (2003)

II.Sera ya Maendeleo na Huduma kwa Watu wenye Ulemavu 2004

Sheria

I.Sheria ya Watu Wenye Ulemavu (Na 9 ya 2010)

Huduma kwa Vyama/Asasi za Watu wenye Ulemavu:

Huduma hii hutolewa kwa Vyama/Asasi za watu wenye ulemavu kwa lengo la kuviwezesha kuboresha uendeshaji wa Vyama/Asasi hizo. Huduma za ushauri hutolewa na Afisa Ustawi wa Jamii katika ngazi ya Wilaya hadi kata

Huduma hii hutolewa kwa:

Kutoa ushauri kwa vyama/asasi za watu wenye ulemavu.


Kuvijengea uwezo ili kutoa huduma madhubuti kwa wanachama wao.


 Kuvipatia ruzuku li vitoe huduma bora kwa wanachama wao

Kutoa ushauri wa kitaalamu.


Huduma za ushauri kwa Wazee:

Huduma hii hutolewa kwa wazee mmoja mmoja au vikundi kwa lengo la kuwawezesha wazee kuishi maisha yaliyo bora.

Maeneo ya ushauri ni pamoja na namna ya kuanzisha/kuendesha miradi ya uzalishaji mali na upatikanaji wa mikopo na masoko ya bidhaa zinazozalishwa.





Matangazo

  • TANGAZO LA ZABUNI YA KUWEKEZA KATIKA ENEO LA BADECO February 04, 2021
  • NAFASI ZA KAZI. 1. WAANDIKISHAJI WAPIGA KURA 167. 2. WAANDIKISHAJI WA AKIBA 167. September 11, 2019
  • Tangazo la nafasi za kazi Halamashauri ya wilaya Bagamoyo 2020. January 24, 2020
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI AFISA MWANDIKISHAJI MSAIDIZI NA BVR OPERATOR BAGAMOYO DC TAREHE 09/01/2020 February 07, 2020
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • ZAIDI YA MILIONI 200 KUTUMIKA KUANDAA MPANGO KABAMBE (MASTER PLAN)

    February 26, 2021
  • LINDENI MISITU YA MIKOKO:WAZIRI UMMY

    February 17, 2021
  • DC KAWAWA AAGIZA TARURA KUONDOA VIFUSI VYOTE BARABARANI

    February 02, 2021
  • BILIONI 41,860,877,939/- ZAPITISHWA KUWA BAJETI KUU YA HALMASHAURI YA WILAYA YA BAGAMOYO

    January 29, 2021
  • Angalia zote

Video

KAULI YA RAIS MAGUFULI WAKATI AKIZINDUA BARABARA YA BAGAMOYO - MSATA
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 023 - 2440164

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo