• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Divisheni na Vitengo
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TASAF
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Usimamizi wa Usafi na Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha mawasiliano Serikalini
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2024-2025
      • Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

MEFADA MKOMBOZI WA WARAIBU WA DAWA ZA KULEVYA BAGAMOYO

Posted on: May 22nd, 2020

Asasi isiyo ya Kiserikali ya MEFADA (Methadone Family Against Drugs Abuse), imefanya utambulisho rasmi wa asasi hiyo pamoja na uzinduzi wa shughuli zake Wilayani Bagamoyo leo, ili jamii ya Bagamoyo ianze kufaidika na huduma zitolewazo na Asasi hiyo.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Asasi hiyo Ndg. Alex Chitawale amesema Asasi hiyo inajishughulisha na utoaji elimu juu ya madhara yatokanayo na dawa za kulevya, UKIMWI, homa ya ini n.k

“Tuna lengo la kuona jamii yetu hasa vijana wakiishi bila kutumia dawa za kulevya na wale ambao wameshaingia katika tatizo hili wakipata usaidizi wa kitaaluma kama vile, tiba, ushauri nasihi na huduma zingine” Amesema Ndg. Chitawale

Anaongeza “Tangu kuanza kwa shughuli za Asasi yetu hapo Mwaka 2015 mpaka sasa tumeshatoa elimu katika Mikoa ya Dar Es Salaam, Dodoma na Pwani, ambapo kwa Dar Es Salaam walengwa 2100 wamefikiwa, Dodoma walengwa 157 na sasa Bagamoyo tuna walengwa 51 ambao wananufaika na huduma zetu, aidha tumejikita pia kutoa elimu ya madhara yatokanayo na dawa za kulevya katika Shule za Sekondari, kuwatafuta na kuwafikia waraibu wa dawa za kulevya na kuwaunganisha na matibabu ya methadone, tumefanya vikao na waathirika wa dawa za kulevya vyenye ushawishi wa waraibu kufikiria kubadilika na kuachana na matumizi ya dawa za kulevya, pia tumefanya vikao vya ngazi za familia (Family Therapy) hususani kwa familia ambazo zina watu waliojiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya ili kuwajengea uwezo wa namna ya kuwahudumia waraibu wanaoishi nao katika familia zao”

Wakati huo huo, Mtaalam toka tume ya uratibu na udhibiti wa dawa za kulevya Nchini   Bi. Salome Mbonile akizungumza katika uzinduzi huo amesema Asasi ya MEFADA ni moja kati ya Asasi ya kiraia wanayofanya kazi nayo na imeonesha matokeo Chanya katika kuisaidia jamii kuondokaa na matumizi ya dawa za kulevya kwa kuwahamasisha waraibu kujiunga na matibabu ya methadone hivyo kuomba Wananchi wa Bagamoyo kushirikiana nayo kwa karibu ili kuunga mkono mapambano dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya Wilayani hapa.

Nae Afisa Tawala (W) Bi. Zubeda Omari ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Mhe. Zainab Kawawa amewakaribisha wataalam wa Asasi hiyo kufanya kazi Wilayani Bagamoyo huku akipongeza shughuli za Asasi hiyo na kuahidi ushirikiano mkubwa toka Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo katika mapambano dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya ili kuikomboa jamii ya Bagamoyo toka katika matumizi ya dawa hizo ambazo ni tishio kwa jamii hususani vijana ambao  ndio nguvu kazi ya Taifa.

Asasi ya MEFADA inafanya kazi Wilayani Bagamoyo katika Kata ya Magomeni, Kitongoji cha Maji Coast Mtaa wa Majengo na Wananchi wanaweza kufika katika Ofisi zao ili kupata huduma zitolewazo na Asasi hiyo.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUTEULIWA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 AWAMU YA PILI... May 09, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA BAGAMOYO... February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA OBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.. February 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI... July 14, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • BAGAMOYO KUJITANGAZA KIMATAIFA SEKTA YA UTALIII...

    May 10, 2025
  • HALMASHAURI YA BAGAMOYO YAPANDA MITI 500 ENEO LA MNADA WA ZINGA KUBORESHA MAZINGIRA...

    April 15, 2025
  • TUTAENDELEA KUSIMAMIA KWA DHATI NA HAKI MISINGI YA DEMOKRASIA...

    April 02, 2025
  • ELIMU KUHUSU MPOX YATOLEWA KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI...

    March 20, 2025
  • Angalia zote

Video

SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 0733860575

    Simu ya kiganjani: 0733860575

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo