• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
    • Baraza la Madiwani
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
      • Baraza la Madiwani
        • Historia
        • Dhima na Dira
        • Muundo wa Taasisi
        • UKARIBISHO
        • service one
        • what we do
        • Utalii
        • Kaole Snake Park
        • Kaole Mamba Ranch
        • Completed
        • Elimu
        • Afya
        • Maji
        • Caravan Serai
        • Education
        • Ukaguzi wa Ndani
        • TAARIFA YA O& OD
        • Miradi iliyopendekezwa
        • Bajeti ya Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo
        • Maendeleo ya Jamii
        • Elimu Msingi
        • Elimu Sekondari
        • Ujenzi
        • Mfuko wa Jamii
        • Mifugo na Uvuvi
        • Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
        • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
        • Idara ya Maji
        • Sheria ndogo za Halmashauri
        • Ardhi na Mipango Miji
        • Idara ya Ujenzi na Zimamoto
        • Sheria
        • Ufugaji Nyuki
        • Usafishaji na Mazingira
        • Fedha na Biashara
        • Election Unit
        • Ugavi na Manunuzi
        • Maeneo ya Uwekezaji
        • TEHAMA na Uhusiano
        • Kupata Fomu Mbalimbali
        • Madiwani
        • Baraza la Madiwani
        • Orodha ya Wahe.Madiwani
        • Kamati za kudumu za Halmashauri
          • Elimu, Afya na Maji
          • Fedha, Uogozi na Mipango
          • Kamati ya UKIMWI
          • Kamati ya Maadili
          • Uchumi, Ujenzi, Mipango miji na Mazingira
        • Ratiba za Vikao vya Kisheria
        • Ratiba
          • Kuonana na Mhe. Mwenyekiti
          • Ratiba ya Vikao vya Wahe. Madiwani
        • Mpango Mkakati
        • Bajeti ya Halmashauri
        • Mkataba wa huduma kwa Mteja
        • ZABUNI MBALI MBALI ZA UWAKALA
    • Baraza la Madiwani
  • Idara na Vitengo
    • Mifugo na Uvuvi
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Elimu Sekondari
      • Works
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Usafi na Mazingira
      • Fedha na Biashara
      • Maji
      • Elimu Msingi
    • Kitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Election Unit
      • TEHAMA na Uhusiano
  • Huduma
    • Elimu
    • Afya
    • Maji
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2018/2019
    • Mkataba wa huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MPYA
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

Usafishaji na Mazingira

Idara ya Usafi na Mazingira inasimamiwa na Kaimu Mkuu wa Idara hiyo Ndg.Cleophace Murugwa.

Simu Na. 0652 648 222


SERA, SHERIA NA KANUNI ZINAZOIONGOZA IDARA YA USAFI NA MAZINGIRA

Idara ya usafi na mazingira inafanya shughuli zake kwa mujibu wa sera, sheria na kanuni zilizoanzishwa na kupitishwa na serikali.

Idara inatekeleza sheria tofauti katika majukumu yake ikiwa ni;-


•Sheria ya Usimamizi wa Mazingira namba 20 ya mwaka (2004) na Kanuni zake za mwaka 2009

•Sheria ndogo ya hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo ya mwaka 2016

•Sheria ndogo za usafi wa mazingira za Halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo mwaka 2016

•Sheria ndogo zilizoanzishwa na zitakazoanzishwa na Halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo.


UTENDAJI KAZI

Majukumu ya Idara hii ni kusimamia utunzaji/Uhifadhi wa Mazingira na Bioanuai, udhibiti wa uchafuzi wa Mazingira (Ardhi, maji, hewa na sauti, na kusimamia usafirishaji na ukusanyaji wa taka ngumu kutoka kwenye ,majengo, maeneo ya wazi, barabara na mifereji ya kuondoa maji ya mvua na maji taka mijini katika makazi.

VITENGO NA KAZI ZAKE


i.    Hifadhi ya Mazingira

•Kutenga maeneo ya upandaji wa miti, majani, maua,ukatiaji wa miti na upendezeshaji wa mazingira.

•Kuhamasisha jamii kushiriki kupanda miti, majani,  maua ukatiaji wa miti na upendezeshaji wa mazingira.

•Kuandaa na kufuatilia utekelezaji wa mipango ya halmashauri ya usimamizi wa mazingira kwa kuzingatia mpango kazi wa Taifa na usimamizi wa Mazingira.

•Kusimamia utekelezaji wa sera ,sheria na miongozo ya kulinda mazingira.

•Kuandaa taarifa ya hali ya mazingira.

•Kusimamia utunzaji wa vyanzo vya maji kwa kudhibiti utekelezaji wa shughuli yoyote inayoweza kuleta athari.

•Kutoa elimu ya hifadhi endelevu ya bioanuari.

•Kuweka na kusimamia mikakati ya kuongoa ardhi iliyoharibiwa na kuzuia uharibifu wa bioanuai.

•Kuhamasisha matumizi yateknolojia ya nishaji mbadala pamoja na majiko banifu.


ii.Udhibiti uchafuzi wa Mazingira( Ardhi, maji, hewa na sauti)

•Kutoa elimu kwa jamii kuhusu njia bora za kudhibiti uchafuzi wa mazingira.

•Kusimamia Sheria za kudhibiti uchafuzi wa Mazingira

•Kusimamia na kudhibiti uchafuzi wa mazingira unaosababishwa na maji taka

•Kufuatilia na kufanya tathmini kwa athari za uchafuzi wa mazingira katika makazi, viwanda, migodi, ujenzi, biashara, kilimo, na ufugaji.


iii.    Tathmini ya athari kwa  mazingira (EIA)

a)    Kusimamia Sheria , Kanuni na Miongozo mbalimbali ya kufanya tathmini kubaini na kuzuia   athari kwa  mazingira

b)    Kufuatilia utekelezaji wa mpango na maelekezo ya tathmini ya athari za mazingira kwa kila mradi uliofanyiwa tathmini hiyo.

c)    Kuratibu utekelezaji wa kazi za kamati za mazingira na kamati za kudumu za halmashauri.

iv.    Udhibiti wa taka ngumu (Solid  Waste Management)

a)    Kusimamia uhifadhi wa muda,uchambuzi na usafirishaji wa taka ngumu.

b)    Kusimamia uendeshaji wa dampo.

c)    Kusimamia uteketezaji wa taka ngumu na taka maji.


HALI YA WATUMISHI

Idara ina mtumishi 1 anayewajibika kwa vitengo vyote. Aidha taratibu za kuongeza watumishi zinaendelea.


MUUNDO WA IDARA

Idara ya Usafi na Mazingira imegawanyika katika vitengo viwili yaani kitengo cha USAFI na kitengo cha MAZINGIRA.


HIFADHI YA MAZINGIRA

Kitengo hiki kina wajibika kutekeleza majukumu mbalimbali kama ifuatavyo;


•kuhakikisha utekelezaji wa Sheria ya usimamizi wa mazingira kwenye eneo zima la Halmashauri ya Bagamoyo.

•Kushauri Menejiment na Kamati ya Usimamizi wa Mazingira ya Halmashauri kuhusu njia sahihi za kuhifadhi mazingira.

•Kutoa elimu ya uifadhi maliasili na Mazingira kwenye Halmashauri ya Bagamoyo.

•Kusimamia na kuratibu mipango kuhusu mazingira na matumizi ya maliasili ndani ya Halmashauri

•Kusimamia taarifa mbali mbali za Tathmini ya Athari kwa Mazingira (EIA) kwa ajili ya uwekezaji wa ndani wa miradi mbalimbali

•kufanya mapitio ya sheria ndogo zinazohusu usimamizi wa mazingira na shughuli maalumu za kisekta zinazohusiana na mazingira;

•kutoa taarifa kwa Mkurugenzi wa Mazingira na Mkurugenzi Mkuu kuhusu utekelezaji wa Sheria ya usimamizi wa mazingira.

•Kutoa Elimu ya Hifadhi ya Mazingira kwa wadau mbalimbali.

•Kushiriki katika kuandaa mpango kazi na Bajeti.

•Kushiriki katika tafiti zinazohusu usimamizi na Hifadhi ya Mazingira.

•Kufuatilia na kuainisha maeneo yanayopaswa kuhifadhiwa.


B: KITENGO CHA USAFI WA MAZINGIRA

Kitengo cha usafi wa Mazingira na taka ngumu kinatekeleza majukumu yafuatayo;-

•kuratibu zoezi la ukusanyaji wa taka ngumu na kuzitupa kwenye maeneo tengwa eg.dampo.

•Kuratibu zoezi la utupaji wa taka maji katika halmashauri ya Bagamoyo.

•Kusimamia utekeleza wa sheria, sera, taratibu na miongozo mbalimbali ya kusafisha mji.

•Kukusanya na kuondoa takataka na kuzipeleka Dampo.

•Kuhakikisha takataka zinatekeketezwa ipasavyo.

•Kusimamia Dampo.


 MIKAKATI YA IDARA

Mikakati hiyo ni pamoja na;-


1. Kuhakikisha kwamba elimu juu ya Hifadhi ya mazingira na afya ya jamii kwa wadau mbalimbali inafanyika mara kwa mara ilikupunguza au kuondoa kabisa tatizo la uharibifu wa mazingira magonjwa ya milipuko katika Wilaya.

2. kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa sheria ya usimamizi wa mazingira no 20 ya 2004 na marekebisho yake ya 2016 dhidi ya waharibifu wa mazingira, na ukiukwaji wa sheria ya afya ya jamii na 1 ya 2009 dhidi ya wale wote wanaoenda kinyume na kanuni, taratibu na miongozo ya afya ya jamii.

3. Kufuatilia na kuainisha maeneo yanayopaswa kuhifadhiwa kama maeneo yenye chepechepe za maji (Aridhi oevu), kandokando mwa kingo za mito, milima ya hifadhi ya jamii, na maeneo mengine yenye thamani mbalimbali ya uhifadhi.

4. Kuboresha taaluma ya watumishi pamoja na maslahi.

5. kuandaa mikakati na mipango mbalimbali ya uhifadhi na utunzaji wa mazingira kama programu za upandaji miti.

6. kufuatilia maandalizi, mapitio na vibali vya Tathmini za athari za mazingira zina fanyika kwa miradi mikubwa ya uwekezaji kama vile miradi ya ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji, Mashule, Minara, uchimbaji wa madini na pia wachimbaji wadogo wa madini kuhakikisha wana mipango ya ulinzi wa mazingira (EPP) na mipango ya usimamizi wa mazingira yaani (EMP) kwa mujibu wa sheria ya usimamizi wa Mazingira na 20 ya 2004 na sheria ya madini na 14 ya 2010.

7. Kuunda kamati za kuhifadhi mazingira kuanzia ngazi ya vijiji,kata na wilaya pamoja na klabu za mtoto kwa mtoto mashuleni.

8. Kuendelea kutoa elimu ya uhifadhi wa mazingira na mabadiliko ya tabia nchi kwa viongozi, watendaji na kamati za Mazingira.





Matangazo

  • TANGAZO LA ZABUNI YA KUWEKEZA KATIKA ENEO LA BADECO February 04, 2021
  • NAFASI ZA KAZI. 1. WAANDIKISHAJI WAPIGA KURA 167. 2. WAANDIKISHAJI WA AKIBA 167. September 11, 2019
  • Tangazo la nafasi za kazi Halamashauri ya wilaya Bagamoyo 2020. January 24, 2020
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI AFISA MWANDIKISHAJI MSAIDIZI NA BVR OPERATOR BAGAMOYO DC TAREHE 09/01/2020 February 07, 2020
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • LINDENI MISITU YA MIKOKO:WAZIRI UMMY

    February 17, 2021
  • DC KAWAWA AAGIZA TARURA KUONDOA VIFUSI VYOTE BARABARANI

    February 02, 2021
  • BILIONI 41,860,877,939/- ZAPITISHWA KUWA BAJETI KUU YA HALMASHAURI YA WILAYA YA BAGAMOYO

    January 29, 2021
  • kikao maalumu cha kamati ya wataalamu C.M.T kupokea na kujadilimmapitio ya mpango na bajeti kwa mwaka 2020/2021 na mapendekezo ya bajeti ya mwaka 2021/2022.

    January 25, 2021
  • Angalia zote

Video

KAULI YA RAIS MAGUFULI WAKATI AKIZINDUA BARABARA YA BAGAMOYO - MSATA
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 023 - 2440164

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo