• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Divisheni na Vitengo
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TASAF
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Usimamizi wa Usafi na Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha mawasiliano Serikalini
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2024-2025
      • Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

DC KAWAWA AWAHAKIKISHIA WANANCHI WA NYAKAHAMBA KEREGE NA MAPINGA KUANZA KUPATA MAJI SAFI IFIKAPO NOVEMBA, 2021

Posted on: November 24th, 2020

DC KAWAWA AWAHAKIKISHIA WANANCHI WA NYAKAHAMBA KEREGE NA MAPINGA KUANZA KUPATA MAJI SAFI IFIKAPO NOVEMBA, 2021.

Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Mhe.  Zainab Kawawa amewahakikishia wakazi wa Kitongoji cha Nyakahamba - Kerege na Vitongozi vya Kibosha, Kimere na Mingoi vya Kata ya Mapinga kuanza kupata huduma Bora za Maji safi ifikapo Mwezi Novemba 2021.

Mhe. Zainab akizungumza katika Mkutano na Wananchi wa Nyakahamba, katika mkutano uliofanyika katika Ofisi za Kitongoji hicho, Novemba 24, 2020, amesema kadhia ya ukosefu wa Maji katika Vitongoji hivyo vya kata ya Kerege na Mapinga itafika tamati hivi karibuni baada ya kukamilika kwa mradi mkubwa wa ujenzi wa busta pump stesheni na tanki la maji la Ujazo wa lita Milioni 05 linalojengwa katika eneo la Vikawe.

“Nitumie fursa hii kuwahakikishia Wananchi wa Kata ya Kerege na Mapinga kuwa shida ya maji itafika mwisho baada ya kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa tanki kubwa la maji lenye ujazo wa lita Mil. 05, na usambaaji wa miundombinu ya mabomba katika makazi ya wananchi wa maeneo hayo, hivyo wawe na subira kwani utekelezaji wa mradi huo unaotekelezwa na DAWASA, unandelea kwa kasi na utakapokamilika kero ya ukosefu wa maji itabaki kuwa historia”. Amesema Mhe. Zainab.

Mhe. Zainab akiambatana na Kamati ya Ulinzi na usalama ya Wilaya, Watendaji wa mamlaka ya DAWASA na RUWASA Wilayani Bagamoyo, wamefanya ziara maalumu ya ukaguzi wa miradi ya maji inayotekelezawa na mamlaka hizo mbili katika Wilaya ya Bagamoyo, ambapo wameshuhudia Mradi wa Ujenzi wa tanki la maji lenye uwezo wa kupokea lita milioni 05 kwa siku likiwa katika hatua ya Msingi.

Aidha, Mhe. Zainab, amewapongeza DAWASA Mkoa wa Bagamoyo, kwa juhudi wanazofanya na kuwaagiza kuongeza kasi ili Mradi huo ukamilike kwa wakati sahihi na kuanza kutoa huduma kwa jamii, kwani mradi huo unatarajiwa kuwanufaisha wakazi takribani 12,000 katika maeneo hayo.

Kwa upande wake Meneja Dawasa Mkoa wa Bagamoyo Bi. Judith Singinika, amesema watahakikisha wanausimamia mradi huo vizuri ili ukamilike kwa wakati na katika viwango vinavyotakiwa.

Wakati huo huo, Mhe. Zainab ametembelea na kukagua miradi ya maji inayotekelezwa na RUWASA Wilayani Bagamoyo, katika Kata ya Yombo na Kata ya Makurunge.

Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini – RUWASA Wilaya ya Bagamoyo, Mhandisi James Kionaumela amesema katika Kata ya Yombo Kitongoji cha Chombejuu wanatekeleza mradi wa upanuzi wa kisima chenye urefu wa Mita 100, chenye uwezo wa kuzalisha lita 7200 kwa saa, ujenzi wa tanki la kuhifadhia maji lenye ujazo wa lita 28,000, ujenzi wa wa kituo kimoja cha kutekea maji chenye koki 8 na ujenzi wa sehemu ya kunyweshea mifugo, mradi utakaowanufaisha takribani wakazi 500 wa eneo hilo.

Mhandisi James anaongeza kuwa, RUWASA katika Kitongoji cha Kuluwi, Kata ya Yombo, inatekeleza mradi wa ujenzi wa Tanki la maji la lita za ujazo 75,000 la mnara wa Mita 6, Ujenzi wa vituo vya kuchotea maji 06, uchimbaji na ulazaji wa bomba la urefu wa Kilomita 2.75, mradi utakaokamilika Mwezi Januari 2021 na unatarajiwa kuwanufaisha wakazi takribani 1623 wa eneo hilo.

Halikadhalika, Mhandisi James Kionaomela ameongeza kuwa RUWASA pia ipo katika utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa tanki la ujazo wa lita 50,000 juu ya mnara wa Mita 12, Vituo 8 vya kuchotea maji, Uchimbaji, ulazaji na ufungaji wa mabomba umbali wa km 5.25 na uunganishaji wa maji kutoka bomba la maji DAWASA Chalinze, miradi inayoendelea kutekelezwa sasa katika Kitongoji cha Mtoni, Makurunge, mradi utakaowanufaisha takribani wakazi 1169 wa eneo hilo.

Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Mhe. Zainab Kawawa ametembelea muradi hiyo yote inayotekelezwa na RUWASA na DAWASA, katika Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, yenye lengo la kuongeza upatikanaji wa huduma ya maji katika maeneo husika.



Matangazo

  • TANGAZO LA KUTEULIWA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 AWAMU YA PILI... May 09, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA BAGAMOYO... February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA OBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.. February 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI... July 14, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • HALMASHAURI YA BAGAMOYO YAPANDA MITI 500 ENEO LA MNADA WA ZINGA KUBORESHA MAZINGIRA...

    April 15, 2025
  • TUTAENDELEA KUSIMAMIA KWA DHATI NA HAKI MISINGI YA DEMOKRASIA...

    April 02, 2025
  • ELIMU KUHUSU MPOX YATOLEWA KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI...

    March 20, 2025
  • WAPENI ELIMU WANANCHI KUHUSU UGOJWA WA MPOX...

    March 17, 2025
  • Angalia zote

Video

SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 0733860575

    Simu ya kiganjani: 0733860575

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo