• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Divisheni na Vitengo
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TASAF
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Usimamizi wa Usafi na Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha mawasiliano Serikalini
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2024-2025
      • Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

AZANIA WAFUTIWA HATI YA UMILIKI WA ARDHI MAPINGA..

Posted on: February 27th, 2023

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amebatilisha,na kutengua umiliki wa shamba namba 934 lililokuwa mali ya AZANIA Investment and management Services Ltd, kitongoji cha Kiembeni Kata ya Mapinga, Bagamoyo Mkoani Pwani ,lenye ukubwa wa hekari 374 na kuamua kulirejesha Serikalini .

Eneo hilo liliingia katika mgogoro mkubwa na wananchi wavamizi ambapo awali AZANIA alitambulika ni mmiliki halali lakini mwishoni mwa wiki Rais Samia ilimpendeza kubatilisha eneo hilo.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani alhaj Abubakar Kunenge,akiwa katika muendelezo wa ziara yake kata ya Mapinga, kutatua migogoro iliyokithiri kata ya Mapinga, alieleza kutokana na kutenguliwa kwa umiliki wa AZANIA kitongoji cha Kiembeni, inatafsiriwa wananchi bado ni wavamizi.

“Kwasasa tuendelee kumuombea mh Rais, kwani akiona imempendeza kutoa maelekezo eneo hili kuwa la makazi mtashukuru,lakini kubatilishwa kwake sio uhalali wa kujimilikisha maeneo mliyovamia”

.”Pabaki kama palivyo ndio Maamuzi ya Serikali,msiendeleze kujenga,mtajiingiza katika hatari,muwe na subira “.

Kunenge alieleza kuwa, na endapo kama Rais ataelekeza liwe eneo la makazi litákuwa Halmashauri ili eneo lipangwe.

Mkuu huyo wa mkoa, alifafanua hakuna aliye juu ya sheria, kwa wale wote waliohusika na uuzaji holela na utapeli wa viwanja Mapinga wachukuliwe hatua za kisheria.

“Nimedhamiria kupiga kambi hapa, kuisafisha kata hii, na kukomesha uuzaji holela wa maeneo,kwa kufuata maelekezo ya kamati iliyoundwa na Waziri wa Ardhi Angelina Mabula,na nitahakikisha nayasimamia Maamuzi ya kamati hiyo na Serikali “alieleza Kunenge.

Nae Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo,Muharami Mkenge alieleza ni wakati wa kufanya maendeleo mengine na atahakikisha migogoro ya ardhi Mapinga na Makurunge inapungua.

Alisema ,Eneo la Greenwood  ,lenye ukubwa wa hekari 5,000 pamoja na shamba la JENETA yote yaliyopo Makurunge,sanjali na kiwanja kimoja kilichopo kata ya Kisutu vimerudishwa Serikalini kwa ajili ya shughuli na maelekezo atakayoelekeza Rais.

Mkenge alisema,tangu mwaka 2021 alianza kusimamia kero hizo,na sasa kata ya Makurunge matokeo yameanza kuonekana.

Awali Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Halima Okash alitoa rai kwa Wananchi kuacha kuuza ardhi kiholela na yeyote aliyeuziwa ardhi apate hati ya halali ili kujiepusha na migogoro.

“Huwa nasikiliza kero za wananchi kila Jumanne na Ijumaa na asilimia 99.9 ya malalamiko nayofikishiwa ni migogoro ya ardhi,”hili ni tatizo kubwa katika wilaya yetu na nitahakikisha nalishughulikia “alieleza Okash.

Kwa upande wa wananchi,mzee Bole Shindika alisema msimamo wa Serikali lazima uheshimiwe, wanashukuru Rais kwa hatua ya kwanza aliyoichukua na wanasuubiri muongozo wake.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUTEULIWA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 AWAMU YA PILI... May 09, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA BAGAMOYO... February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA OBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.. February 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI... July 14, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • BAGAMOYO KUJITANGAZA KIMATAIFA SEKTA YA UTALIII...

    May 10, 2025
  • HALMASHAURI YA BAGAMOYO YAPANDA MITI 500 ENEO LA MNADA WA ZINGA KUBORESHA MAZINGIRA...

    April 15, 2025
  • TUTAENDELEA KUSIMAMIA KWA DHATI NA HAKI MISINGI YA DEMOKRASIA...

    April 02, 2025
  • ELIMU KUHUSU MPOX YATOLEWA KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI...

    March 20, 2025
  • Angalia zote

Video

SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 0733860575

    Simu ya kiganjani: 0733860575

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo