• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Divisheni na Vitengo
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TASAF
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Usimamizi wa Usafi na Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha mawasiliano Serikalini
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2024-2025
      • Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

BAGAMOYO YATEKELEZA MAFUNZO YA UANDAAJI WA MIPANGO NA BAJETI ZA AFUA ZA LISHE KWA HALMASHAURI

Posted on: December 12th, 2019

Katika kuhakikisha kwamba hali ya lishe katika Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo inaboreka hasa lishe ya mama na mtoto, Halmashauri imeendesha mafunzo maalum kwa wataalam wa kisekta wa Halmashauri yaliyohusu uandaaji wa mipango na bajeti za afua za lishe kwa Halmashauri kwa Mwaka wa fedha 2020/2021.

Mafunzo hayo yaliyohusu namna bora za uwekaji vipaumbele za masuala ya lishe katika mpango na bajeti ya Halmashauri yamefunguliwa rasmi na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Mhe. Zainab Kawawa mapema tarehe 12/12/2019, katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo.

Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo Mhe. Zainab Kawawa amesema ni muhimu kwa jamii kutambua umuhimu wa kuzingatia lishe bora kwa mama na mtoto pia lishe ya watu wazima ili kuondokana na tatizo la utapimlo mkubwa uliokithiri katika jamii zetu kwa watu kutozingatia lishe bora.

“Tukiweza kudhibiti lishe duni katika jamii yetu, itasaidia kuleta maendeleo katika jamii yetu, kwani jamii yenye lishe duni haiwezi kushiriki katika shughuli za maendeleo kutokana na mwili kukosa afya na nguvu ya kufanya kazi na wakati mwingine kushambuliwa na magonjwa” Amesema Mhe. Zainab Kawawa

Ameongeza, Azma ya Serikali ni kuhakikisha jamii inafahamu juu ya umuhimu wa lishe bora na uzingatiaji wa lishe bora katika kukabiliana na tatizo la utapiamlo Nchini, hivyo amewaasa wataalam washiriki wa mafunzo hayo kuzingatia vipaumbele vya Serikali katika masuala ya lishe ya jamii wakati wa maandalizi ya mpango na bajeti wa Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2020/2021 huku akisisitiza utoaji wa elimu kwa wananchi juu ya masuala ya lishe.

Tafiti mbalimbali zilizofanywa na taasisi ya chakula na lishe Nchini, (TFNC) ambao pia wamewezesha mafunzo hayo, zinaonesha kumekuwa na tatizo kubwa la utapiamlo uliokithiri si kwa watoto tu bali hata kwa watu wazima kwani wengi wao hawazingatii lishe bora.

Ili kukabiliana na tatizo hili kubwa la utapiamlo kwa watoto na watu wazima, Serikali kupitia Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, inayosimamia Halmashauri zote Nchini imeandaa mafunzo haya maalum yanayofanyika katika Halmashauri zote ili wakati Halmashauri zinaandaa mpango na bajeti wa Halmashauri husika ihakikishe inazingatia vipaumbele vya masuala ya lishe ili kuboresha hali ya lishe katika Halmashauri husika.

Mafunzo haya ya uandaaji wa mipango na bajeti za afua za lishe kwa Halmashauri yamefanyika kwa siku moja na yamehudhuriwa na wataalam wa kisekta toka Idara ya Afya, Mifugo na Uvuvi, Kilimo, Elimu Sekondari na Msingi, Maendeleo ya Jamii, Mipango na Takwimu, wawakilishi toka asasi za kiraia na wawezeshaji toka OR – TAMISEMI, Taasisi ya chakula na lishe (TFNC) na Mratibu wa lishe Mkoa wa Pwani.




Matangazo

  • TANGAZO LA KUTEULIWA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 AWAMU YA PILI... May 09, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA BAGAMOYO... February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA OBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.. February 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI... July 14, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • HALMASHAURI YA BAGAMOYO YAPANDA MITI 500 ENEO LA MNADA WA ZINGA KUBORESHA MAZINGIRA...

    April 15, 2025
  • TUTAENDELEA KUSIMAMIA KWA DHATI NA HAKI MISINGI YA DEMOKRASIA...

    April 02, 2025
  • ELIMU KUHUSU MPOX YATOLEWA KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI...

    March 20, 2025
  • WAPENI ELIMU WANANCHI KUHUSU UGOJWA WA MPOX...

    March 17, 2025
  • Angalia zote

Video

SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 0733860575

    Simu ya kiganjani: 0733860575

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo