• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Divisheni na Vitengo
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TASAF
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Usimamizi wa Usafi na Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha mawasiliano Serikalini
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2024-2025
      • Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

BANDARINI KUCHELE, WAFANYABIASHARA WAANZA KUSHUSHA KWA KASI MIZIGO BANDARI YA BAGAMOYO

Posted on: June 5th, 2020

Ikiwa ni siku moja tu tangu Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo afanye Mkutano maalum na wafanyabiashara wanaotumia bandari ya Bagamoyo, waliokuwa wameikacha bandari hiyo, na kuwasihi wafanya biashara hao kuanza kutumia bandari hiyo kama ilivyo kuwa awali, jana jioni majahazi mawili yenye shehena ya mafuta yaliingia katika bandari hiyo, ikiwa ni ishara ya kuisha kwa mgomo wa kutoitumia bandari hiyo uliowekwa na wafanya biashara hao kwa takribani kipindi cha miezi mitatu iliyopita.

Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Zainab Kawawa alishirikiana na wafanyabiashara hao kuyapokea majahazi hayo yaliyotokea Zanzibar yakiwa na shehena ya mafuta ya kula aina ya OKI yakitokea Unguja, huku wafanyabiashara hao wakionesha kufurahishwa sana na kitendo cha Mkuu wa Wilaya kufika bandarini hapo na kushirikiana nao kupokea majahazi hayo.

“Niliahidi kufika hapa leo kushirikiana nanyi kupokea bidhaa ikiwa mngekubali kuanza tena kutumia bandari yenu ya Bagamoyo, na nimetimiza ahadi yangu hiyo, na nimefurahishwa sana kwa ninyi kuitikia kwa vitendo wito wangu wa kurejea katika bandari yenu ya Bagamoyo na kuanza kuitumia tena, bandari  hii ipo kwa ajili yenu, nawasihi endeleeni kuitumia bandari yenu ya Bagamoyo, kero na malalamiko yenu tayari nimeyashughulikia, hakuna atakayewabughudhi tena na atakayejaribu kufanya hivyo Ofisi yangu iko wazi njooni tuzungumze, na nichukue fursa hii kusisitiza suala la wafanya biashara wadogo wanaoutumia bandari hii maarufu kama “shuba shuba” ni marufuku kwa watendaji kuwabughudhi shubashuba tangu leo, waacheni wafanye shughuli zao kwa uhuru wapeni huduma wanazostahili na tendeni haki kwa wafanya biashara wote” Amesisitiza Mhe. Zainab

Baada ya mapokezi hayo bandarini hapo, Mwenyekiti wa Chama cha Wachukuzi katika Bandari ya Bagamoyo Bw. Andrew Nyoni amezungumza na kusema Tumefarijika sana na kufurahishwa sana na kitendo hiki cha Mkuu wetu wa Wilaya ya Bagamoyo kufika hapa leo na kushirikiana nasi kupokea majahazi haya yenye bidhaa za mafuta tuliyoagiza kutoka Unguja, aliahidi kama tukikubali kuagiza mzigo kupitia bandari yetu ya Bagamoyo, basi shehena ya kwanza itakayofika atahakikisha anakuja kushirikiana nasi kupokea mzigo, na kweli leo ametimiza ahadi yake kwa kufika hapa, ni jambo la kufurahisha sana, hii haijawahi kutokea, tumefarijika sana na tunamwahidi Mhe. Mkuu wa Wilaya yetu kuwa kazi ndio imeanza, tupo tayari na tumamua sasa tutaendelea kutumia bandari yetu hii maana ametutia moyo sana kwa kushughulikia kwa haraka mno kero zetu tulizomfikishia hapo juzi, tunamshukuru sana.

Bandari ya Bagamoyo ni moja ya vyanzo vikuu vya Mapato katika Wilaya ya Bagamoyo na kusimama kwa biashara katika bandari hiyo kulipelekea mapato kushuka kwa kiasi kikubwa hali iliyopelekea Mhe. Mkuu wa Wilaya kufanya Mkutano maalum na wafanya biashara wanaotumia bandari hiyo, kusikiliza malalamiko na kero zao kisha kuzitaftia ufumbuzi wa haraka, na kuwasihi wafanya biashara hao kuanza tena kutumia bandari hiyo, jambo lililoitikiwa kwa mlengo chanya na wafanyabiashara hao.



Matangazo

  • TANGAZO LA KUTEULIWA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 AWAMU YA PILI... May 09, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA BAGAMOYO... February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA OBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.. February 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI... July 14, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • HALMASHAURI YA BAGAMOYO YAPANDA MITI 500 ENEO LA MNADA WA ZINGA KUBORESHA MAZINGIRA...

    April 15, 2025
  • TUTAENDELEA KUSIMAMIA KWA DHATI NA HAKI MISINGI YA DEMOKRASIA...

    April 02, 2025
  • ELIMU KUHUSU MPOX YATOLEWA KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI...

    March 20, 2025
  • WAPENI ELIMU WANANCHI KUHUSU UGOJWA WA MPOX...

    March 17, 2025
  • Angalia zote

Video

SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 0733860575

    Simu ya kiganjani: 0733860575

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo