• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Divisheni na Vitengo
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TASAF
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Usimamizi wa Usafi na Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha mawasiliano Serikalini
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2024-2025
      • Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

BILIONI 41,860,877,939/- ZAPITISHWA KUWA BAJETI KUU YA HALMASHAURI YA WILAYA YA BAGAMOYO

Posted on: January 29th, 2021

Baraza la Madiwani la Halmashauri ya wilaya ya Bagamayo leo tarehe 29/01/2021 limepitisha makisio ya mpango wa bajeti ya Halmashauri ya wilaya ya bagamoyo kwa mwaka wa fedha 2021/2022 kiasi cha Tsh.41,860,877,939.00 kati ya fedha hizo Tsh.8,069,195,609 ni ruzuku ya miradi ya maendeleo,Tsh 28,128,366,330 mishahara na Tsh 3,854,020,000 ni mapato ya ndani .

Aidha Halmashauri imeongeza nakisi ya mapato ya ndani kutoka shilingi 3,493,108,000.00.00 hadi kufikia shilingi 3,854,020,000.00 ambalo ni ongezeko la shilingi 360,912,000.00 sawa na asilimia 9 ya bajeti iliyoidhinishwa kutumika katika mwaka wa fedha 2021/2022.

Halmashauri pia imefanya mapitio ambayo yamesaidia kuandaa mpango mkakati mpya wa Halmashauri kwa kipindi cha miaka mitano 2021/2022-2025/26 katika kukuza uchumi kipaumbele cha Halmashauri kitakuwa kuendelea kuimarisha sekta ya kilimo,Mifugo na Uvuvi kwa kuboresha upatikanaji wa mbegu na pembejeo za kilimo pamoja na kujenga na kukarabati miundombinu ya umwagiliaji,masoko na Mifugo na Uvuvi.

Halikadhalika ,Halmashauri katika mwaka wa fedha 2021/2022 itahakikisha inewekeza katika eneo la ufukwe wa bahari ( BADECO) ili kuiwezesha Halmashauri kuongeza mapato ya ndani,Vipaombele katika maendeleo ya watu vitajumuisha Usafi wa mazingira,Afya,Elimu,Ajira na Uendeshaji Ujuzi na Utawala bora na huduma kwa Wananchi.

Halmashauri katika bajeti ya 2021/22 itaendelea kuongeza ufanisi wa utekelezaji wa mpango na bajeti kwa kutekeleza mkakati wa ufuatiliaji na tathimini ya Halmashauri 2020/22-2025/26.pia itaendelea kuwajengea uwezo watumishi wanaohusika na usimamizi,ufatiliaji na tathmini ya miradi ya maendeleo na kuimarisha ushiriki wa wananchi katika utekelezaji wa mipango kwa kutumia dhana na vikwazo kwa maendeleo ili kuboreshwa.

Katika kipindi cha mwaka wa fedha 2020/2021,Halmashauri iliidhinishiwa kukusanya na kutumia jumla ya Tsh. 32,181,594,033.00 hadi kufikia June 2020 Halmashauri ilikuwa imetumia jumla ya Tsh.22,179,656,269.00 sawa na asilimia 69 ya makadirio ya mapato yote yanayojumuisha mapato ya ndani ruzuku ya mishahara,ruzuku ya matumizi ya kawaida na ruzuku ya miradi ya maendeleo.  

Sanjari na hayo Mkurugenzi wa Halamashauri ya wilaya ya Bagamoyo Bi Fatuma  Latu ametoa shukrani kwa namna baraza la Madiwani wameweza kupitia na kutoa maoni yao na kutoa Baraka zote kwa bajeti  hiyo ili iweze kuendelea kwenye vikao husika na hatimae kamati ya bunge kwa ajili ya kuidhinishwa

‘’nipende kutoa pongezi kwa mhe mwenyekiti wa halmashauri,madiwani pamoja wa wakuu wa vitengo waliohudhulia kikao hichi na kupitia pamoja na kutoa maoni yao juu ya bajeti hii na mwisho kupitia kwa mikono yao yote miwili’’alisema Bi Fatuma

Nae Mwanyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Mohamedi Usinga  amemshukuru mkurugenzi mtendaji kwa namna anavyompatia ushirikiano pamoja na wataalamu wake wote,huku pia akiwashukuru watendaji kata katika kipindi wakati wa kutimiza majukumu yao.

Mhe Usinga pia amewaomba waheshimiwa madiwani wote kwa pamoja kufanya kazi kwa ushirikiano wa pamoja ili kuweza kufikia malengo ambayo tayari wameazimia kuyafikia katika kipindi cha mwaka wa fedha 2021/22 na kuwahakikishia kuwapa ushirikiano wa kutosha kama Mwenyekiti wa Halmashauri.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUTEULIWA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 AWAMU YA PILI... May 09, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA BAGAMOYO... February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA OBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.. February 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI... July 14, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • BAGAMOYO KUJITANGAZA KIMATAIFA SEKTA YA UTALIII...

    May 10, 2025
  • HALMASHAURI YA BAGAMOYO YAPANDA MITI 500 ENEO LA MNADA WA ZINGA KUBORESHA MAZINGIRA...

    April 15, 2025
  • TUTAENDELEA KUSIMAMIA KWA DHATI NA HAKI MISINGI YA DEMOKRASIA...

    April 02, 2025
  • ELIMU KUHUSU MPOX YATOLEWA KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI...

    March 20, 2025
  • Angalia zote

Video

SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 0733860575

    Simu ya kiganjani: 0733860575

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo