• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Divisheni na Vitengo
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TASAF
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Usimamizi wa Usafi na Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha mawasiliano Serikalini
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2024-2025
      • Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

CAMFED MKOMBOZI WA WANAFUNZI BAGAMOYO

Posted on: August 27th, 2018



Wanafunzi wa kidato cha kwanza katika Shule za Serikali za Kata ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo wamenufaika kwa kiasi kikubwa, na mradi uitwao English Literacy chini ya programu ya e – readers, programu inayowawezesha kujifunza lugha ya Kiingereza kwa urahisi na ufanisi hivyo kuwasaidia Wanafunzi hao kuelewa kwa urahisi masomo ya Sekondari yanayofundishwa kwa lugha ya Kiingereza, baada ya kumaliza elimu ya Msingi walikokuwa wakisoma masomo yote kwa lugha ya Kiswahili.
Programu ya e – readers katika Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, unatekelezwa katika Shule za Sekondari tano ambazo ni Dunda Sekondari, Matimbwa, Kingani, Hassanal Damji na Zinga Sekondari, zilizopewa vifaa vya kielektroniki 53 vya e - readers kwa kila Shule, huku kigezo kikubwa cha Shule kuingizwa kwenye mradi kikiwa ni kuangalia shule yenye miundombinu ya uhakika ya umeme au chanzo ambacho kinaweza kuchaji vifaa vyenye programu ya e - readers bila matatizo.

E – readers ni programu inayowekwa kwenye kifaa mfano wa simu (tablet), yenye uwezo wa kuhifadhi nyaraka za kujifunzia mfano hadithi, kamusi, n.k zikiwa katika lugha za kiingereza lakini zenye uwezo wa kutafsiriwa na kifaa hicho kwenda katika lugha ya Kiswahili.

Mradi huu unatekelezwa kwa ufadhili wa Shirika lisilo la kiserikali liitwalo CAMFED (Campaign for Female Education) toka Nchini Uingereza, ukiwa na lengo la kusaidia na kuwawezesha wasichana wa Shule za Sekondari hasa Kidato cha Kwanza Nchini kujenga uwezo wa kuielewa lugha inayotumika kufundishia Shule za Sekondari yaani Kiingereza.

Nchini Tanzania CAMFED ilianza rasmi kusaidia wanafunzi kupitia program ya e - readers, mnamo Mwaka 2006 ambapo mradi ulianza utekelezwaji wake katika Wilaya ya Iringa, kisha zikafuata Wilaya za Morogoro Vijijini, kibaha na Tanga, na hadi sasa mradi unatekelezwa katika Wilaya 33 Nchini ikiwa ni pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo.

Mratibu wa program ya e – readers Wilayani Bagamoyo Bi. Diris Martin anabainisha lengo kuu la mradi huu kuwa ni kusaidia wanafunzi wa Sekondari kujifunza lugha ya Kingereza kwa ufanisi hasa Wanafunzi wa kidato cha kwanza, na anakiri kwamba tangu mradi huo uanze kutekelezwa katika Shule tano za Sekondari ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo umeonesha mafanikio makubwa.

“Tunatarajia kuona matokeo mazuri toka kwa Wanafunzi hawa wanaotumia programu ya e – readers watakapokuwa kidato cha Pili, kwani tunaamini Mwanafunzi akielewa vizuri lugha ya kiingereza ni rahisi kwake kuelewa masomo mengine na kufanya vizuri katika mitihani yake” Anasema Bi. Diris

Anaongeza, Programu hii ya English literacy inategemewa iendane na matukio mbalimbali kwa wanafunzi ili kupata matokeo chanya zaidi, lakini pia kuwasaidia Wanafunzi ili wapende lugha ya Kiingereza, hivyo inawalazimu Wanafunzi kufanya mazoezi ya kuzungumza Kiingereza katika utaratibu wa midahalo ya mara kwa mara ya ndani na nje ya shule. Majibizano (dialogue), kusoma na kueleza hadithi kwa lugha ya Kiingereza (story telling) n.k

Nae Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Dunda, moja ya Shule ambazo zinanufaika na programu ya e – readers Bi. Deodata Nkwera, anasema, Programu hiyo ni Mkombozi kwa Wanafunzi sio tu wa kidato cha kwanza Shuleni hapo, ambao mradi uliwalenga zaidi, kwani programu imekuwa msaada mkubwa kwa Wanafunzi wote, kuanzia Kidato cha kwanza, hadi kidato cha nne, na hivyo kutumia fursa hiyo kuwahamasisha Wanafunzi hao kuitumia fursa hiyo vizuri ili mradi huo utakapomaliza muda wake wawe wamenufaika na wamekuwa mahiri wa lugha ya Kiingereza.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Idara ya Elimu Sekondari wa Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo, Bw.Evodius Chilipueli amesema anaipongeza sana taasisi ya CAMFED kwa mradi wao wa e – readers wanaoutekeleza katika Shule tano za Sekondari za Kata za Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo kwani mradi umeonesha mafanikio makubwa kwa Wanafunzi wa kidato cha kwanza hasa waliotoka katika Shule za msingi za Serikali ambako walikuwa wakisoma masomo yote kwa lugha ya Kiswahili kasoro somo la lugha ya Kiingereza.

 “Nawahimiza Wanafunzi wote ambao programu ya e – reader inatekelezwa katika Shule zao kuitumia kwa manufaa, waazime vifaa vya e-readers kwa wingi, wajifunze misamiati mipya ya kiingereza, waongee kwa bidi lugha ya kiingereza wanapokuwa Shuleni na nyumbani bila kuogopa au kuona haya kufanya makosa wakati wanapozungumza kwani kukosea ndio kujifunza” Anasema Ndg. Chilipueli.

Aidha Mwanafunzi Don Anthony, Mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari Dunda anasema programu ya e – readers imemsaidia sana kuunda misamiati mipya ya lugha ya kiingereza, kumjengea ujasiri wa kuzungumza lugha ya kiingereza wanapokuwa katika kipindi cha mdahalo (debate) shuleni, na kupata wepesi wakati wa kuandika insha za masomo mbali mbali kwa Kiingereza.

Nae Mwanafunzi Shumina Molley, Mwanafunzi wa kidato cha Kwanza, Shule ya Sekondari Dunda anasema anaishukuru sana taasisi ya CAMFED kwa kuwaletea programu ya e – readers Shuleni kwao, kwani yeye binafsi imemsaidia kujenga usahihi wa kuongea lugha ya kiingereza bila kukwama kwama kama ilivyokuwa hapo awali na kuwasihi Wanafunzi wenzake kutumia programu hiyo kwani ni msaada mkubwa kwao

Programu ya e – readers itatekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo kwa muda wa miaka miwili, na inatarajiwa kuwanufaisha Wanafunzi wa Sekondari katika Shule za Serikali za Kata wapatao 1800



Matangazo

  • TANGAZO LA KUTEULIWA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 AWAMU YA PILI... May 09, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA BAGAMOYO... February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA OBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.. February 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI... July 14, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • BAGAMOYO KUJITANGAZA KIMATAIFA SEKTA YA UTALIII...

    May 10, 2025
  • HALMASHAURI YA BAGAMOYO YAPANDA MITI 500 ENEO LA MNADA WA ZINGA KUBORESHA MAZINGIRA...

    April 15, 2025
  • TUTAENDELEA KUSIMAMIA KWA DHATI NA HAKI MISINGI YA DEMOKRASIA...

    April 02, 2025
  • ELIMU KUHUSU MPOX YATOLEWA KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI...

    March 20, 2025
  • Angalia zote

Video

SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 0733860575

    Simu ya kiganjani: 0733860575

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo