• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Divisheni na Vitengo
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TASAF
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Usimamizi wa Usafi na Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha mawasiliano Serikalini
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2024-2025
      • Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

DC BAGAMOYO ASISITIZA WELEDI KATIKA UTUMISHI WA UMMA

Posted on: August 28th, 2018



Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Zainabu Mfaume Kawawa, amezungumza na watumishi wa Umma wa Wilaya ya Bagamoyo na kusisitiza uwajibikaji unaozingatia weledi na kujituma pasi na kusubiri kusukumwa na viongozi.
Mhe. Kawawa ameyasema hayo mara baada ya kuitisha kikao maalumu cha kujitambulisha kwa watumishi wa umma wa Wilaya ya Bagamoyo kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo leo Agosti 28, 2018.
“Watumishi nasisitiza kila mmoja wetu atimize majukumu yake kwa kujituma, weledi na kwa kuzingatia wakati, toeni mrejesho wa majukumu na maelekezo mnayopatiwa na viongozi, mnapokutana na changamoto ziwasilisheni kwa wakubwa wenu wa kazi ili wawasaidie kuzitafutia ufumbuzi” amesema Mhe. Kawawa.
Anaongeza kusema kuwa, Serikali ya Awamu ya tano ni Serikali inayofanya kazi kwa kutarajia matokeo chanya, hivyo Watumishi wa umma kila mmoja katika utekelezaji wa majukumu yake ni mtatuzi wa matatizo na kero za wananchi na kwa kufanya hivyo wanalinda heshima ya Serikali na kuleta matokeo chanya kwa Wananchi hasa wanyonge na wa hali ya chini.
Mhe. Kawawa pia, ametumia fursa hiyo kukemea tabia ya Wafugaji wa kimang’ati katika Wilaya ya Bagamoyo kujichukulia sheria mkononi na kuwavamia, kuwapiga wakulima, lakini akakemea pia watumishi wa umma ambao kwa namna moja wanachagiza migogoro ya ardhi na kuongeza kuwa hatasita kuwachukulia hatua kali watumishi watakaobainika kuwa chanzo cha migogoro ya Ardhi Wilayani Bagamoyo.
“Nawaagiza Maafisa ardhi wa Halmashauri za Chalinze na Bagamoyo kuanisha migogoro yote ya ardhi katika maeneo yenu, ikionesha chanzo cha mgogoro, kama imetatuliwa au la na kwa migogoro ambayo haijatatuliwa muoneshe mpango maalumu wa kutatua migogoro hiyo, pia hakikisheni kuwa mnaandaa na kuwasilisha ofisini kwangu mpango wa matumizi bora ya ardhi wa maeneo yote yenye migogoro ya ardhi Wilayani Bagamoyo” Amesema Mhe. Kawawa.
Aidha, Mhe. Kawawa ametaja maeneo sita ya kipaumbele katika uongozi wake akiwa Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo na kuyabainisha kuwa ni kuimarisha ulinzi na usalama wa Wananchi na mali zao, Kusimamia ukusanyaji mapato ya ndani ya Halmashauri, Uongozi shirikishi unaozingatia kushuka hadi ngazi ya chini kabisa kwa Wananchi na kusikiliza kero na matatizo yao na kuyatafutia ufumbuzi wa kudumu, kusimamia na kuendeleza shughuli za maendeleo na kukuza uchumi za vikundi vya Wanawake na Vijana na mwisho ni kuitangaza Bagamoyo kitaifa na Kimataifa kwa kasi hususani vivutio vya kitalii na miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali katika Wilaya ya Bagamoyo.
Nao Wakurugenzi wa Halmashauri mbili zinazounda Wilaya ya Bagamoyo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo Bi. Fatuma Omari Latu na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chalinze Bi. Amina Mohamed Kiwanuka, wamesema wameyapokea maagizo na maelekezo hayo ya Serikali na kwamba wako tayari kusimamia utekelezaji wake huku wakimuahidi Mhe. Kawawa ushirikiano na kumuunga mkono katika kuhakikisha Bagamoyo inapiga hatua katika sekta zote muhimu hususani Sekta za Uchumi, Afya na Elimu.



Matangazo

  • TANGAZO LA KUTEULIWA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 AWAMU YA PILI... May 09, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA BAGAMOYO... February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA OBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.. February 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI... July 14, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • BAGAMOYO KUJITANGAZA KIMATAIFA SEKTA YA UTALIII...

    May 10, 2025
  • HALMASHAURI YA BAGAMOYO YAPANDA MITI 500 ENEO LA MNADA WA ZINGA KUBORESHA MAZINGIRA...

    April 15, 2025
  • TUTAENDELEA KUSIMAMIA KWA DHATI NA HAKI MISINGI YA DEMOKRASIA...

    April 02, 2025
  • ELIMU KUHUSU MPOX YATOLEWA KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI...

    March 20, 2025
  • Angalia zote

Video

SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 0733860575

    Simu ya kiganjani: 0733860575

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo