• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Divisheni na Vitengo
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TASAF
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Usimamizi wa Usafi na Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha mawasiliano Serikalini
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2024-2025
      • Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

DC HALIMA AKABIDHI PIKIPIKI SITA KWA WATENDAJI KATA....

Posted on: February 28th, 2023

Halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo, Mkoani Pwani ,imepokea pikipiki sita kutoka Serikalini kwa ajili ya kuondoa changamoto ya usafiri kwa watendaji kata, ambao wakati mwingine wanashindwa kutekeleza majukumu yao kutokana na baadhi ya maeneo kutofikika kirahisi.

Akikabidhi Pikipiki hizo kwa watendaji kata hao, mkuu wa wilaya ya Bagamoyo,Halima Okash aliwaasa watendaji kuwatumikia wananchi,kwa kutoka Ofisini na kwenda kwenye Maeneo Yao kujua kero zao na kuzitatua.

“Serikali inatambua majukumu na changamoto za watendaji, katika suala zima la usafiri ili kuwarahisishia wafike maeneo ya Vijijini na yaliyo pembezoni mwa miji ,kwa ajili ya kutekeleza majukumu yao” ,twende na Kasi ya Rais Samia Suluhu Hassan ili tusimkwamishe”

“Niwaombe mkazitunze na kuzifanyia kazi mliyotumwa na sio kuzitumia kwenye safari zilizo nje ya wajibu wenu wa kazi ,mkawatumikie wananchi na kuleta matokeo chanya ya kimaendeleo” Changamoto ni maeneo mengine kuwa mbali na kushindwa kufikika kirahisi ,Sasa nendeni mkafanye kazi “alieleza Halima.

Nae Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bagamoyo,Shauri Selenda alieleza , Pikipiki sita zimetolewa na Serikali kwa ajili ya kuwarahisishia usafiri watendaji kwenye kazi zao.

Alieleza ,huo ni mgao wa awamu ya kwanza ,kata zipo 11 hivyo watazigawa katika kata ambazo Zina vijiji vilivyo ndani ,vilivyo na umbali mrefu na awamu ya pili zitaelekezwa kwenye kata zilizobakia.


Selenda alizitaja kata zilizofanikiwa kupata mgao wa kwanza ni pamoja na Kilomo, Zinga, Makurunge, Fukayose,Yombo na Kerege.

Katika hatua nyingine, Halmashauri ya Bagamoyo, imedhamiria kuendelea kuboresha miundombinu mbalimbali ya maji, barabara,na kuweka Mazingira mazuri ili kuvutia wawekezaji na watalii kwenye Mji huo mkongwe.

Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo , Mohammed Usinga ,alitoa maelekezo ya baraza la madiwani na kuitaka Wakala wa misitu( TFS)Bagamoyo kutenga fedha kati ya makusanyo yake makubwa inayokusanya ili kudhibiti uchafuzi wa fukwe (bahari) na kusaidia na Halmashauri.

Alisema ,kwasasa  watalii wamekuwa wakikutana na mpangilio mbovu wa fukwe kwa wafanyabiashara na uchafuzi wa fukwe Hali ambayo inaondoa utulivu kwa watalii.

Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Selenda alieleza ,ipo mipango mkakati ya kuweka maeneo maalum ya kupaki magari , na kupanga wafanyabiashara waliopo pembezoni mwa fukwe .


Hata hivyo,Selenda alieleza , kwasasa wamejipanga kuendelea kuweka Mazingira mazuri ya kuvutia watalii BADECO beach iwe ya kisasa na tayari wamepata wawekezaji,kati ya wawekezaji hao yupo ambae ameshajinasibu kuwekeza kwa milioni 449 ,hali itakayosaidia kuongeza mapato ya halmashauri.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUTEULIWA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 AWAMU YA PILI... May 09, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA BAGAMOYO... February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA OBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.. February 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI... July 14, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • BAGAMOYO KUJITANGAZA KIMATAIFA SEKTA YA UTALIII...

    May 10, 2025
  • HALMASHAURI YA BAGAMOYO YAPANDA MITI 500 ENEO LA MNADA WA ZINGA KUBORESHA MAZINGIRA...

    April 15, 2025
  • TUTAENDELEA KUSIMAMIA KWA DHATI NA HAKI MISINGI YA DEMOKRASIA...

    April 02, 2025
  • ELIMU KUHUSU MPOX YATOLEWA KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI...

    March 20, 2025
  • Angalia zote

Video

SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 0733860575

    Simu ya kiganjani: 0733860575

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo