• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Divisheni na Vitengo
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TASAF
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Usimamizi wa Usafi na Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha mawasiliano Serikalini
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2024-2025
      • Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

DC KAWAWA AFANYA MIKUTANO KUTATUA KERO ZA WANANCHI WA KATA ZA MAGOMENI NA DUNDA

Posted on: June 12th, 2020

Kila siku ya Jumanne Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Mhe. Zainab Kawawa amejiwekea utaratibu wa kusikiliza kero na malalamiko toka kwa wananchi wa Bagamoyo na kuzitaftia ufumbuzi akishirikiana na wataalam wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

Katika kuongeza wigo huo na kupunguza zaidi kama si kumaliza kabisa kero za wananchi, Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Zainab Kawawa, amesogea karibu zaidi na Wananchi kwa kuwafata wananchi hao katika Kata zao na kufanya mikutano maalum ya kuzungumza na Wananchi na kusikiliza kero zao na kuzitatua papo kwa papo

Siku ya tarehe 11/06/2020 Mkuu wa Wilaya amefanya mikutano miwili ya kusikiliza kero za wananchi katika Kata za Magomeni na Dunda ambapo Wananchi wamepata fursa ya kuwasilisha kero na malalamiko yao mbali mbali na Mkuu wa Wilaya kuzitatua papo hapo jambo lililowafurahisha sana Wananchi hao.

Ndg. Mohamed Said Mkazi wa Sanzale katika mkutano huo amelalamikia ukosefu wa Shule ya Msingi katika eneo la Sanzale, jambo linalowafanya watato hao kutembea umbali mrefu kufata huduma ya elimu katika Shule ya Msingi Kidongo chekundu

Ndg. Mohamed Anaongeza, “Mhe. Mkuu wa Wilaya wakazi wa Sanzale tunapata tabu sana na uwepo wa dampo katika eneo la makazi yetu, dampo limejaa sana na taka zinamwagwa barabarani jambo ambalo pia linahatarisha sana afya za wakazi wa Wananchi”

Akijibu kero hizo Mhe. Zainab Kawawa amewataka wakazi wa Sanzale ambao wamepewa eneo lenye ukubwa wa ekari 67 na Mhe Rais Mwaka 2017, kuhakikisha wanatenga ardhi kwa ajili ya miundo mbinu ya huduma za jamii ikiwemo, Shule, zahanati, soko nk, ili Eneo la Sanzale lipate eneo la kujengwa Shule ya Msingi na kumaliza kero hiyo kwa watoto wa maeneo hayo

Kuhusiana na Uwepo wa dampo lililojaa katika maeneo ya makazi ya watu katika eneo hilo, Kaimu Mkuu wa Idara ya Mazingira akizungumza kwa niaba ya Mhe. Mkuu wa Wilaya amesema, mkakati wa muda mfupi wa kukabiliana na kero ya dampo katika eneo hilo ni kuhakikisha taka zinasambazwa kila baada ya miezi mitatu, aidha Halmashauri katika bajeti ya Mwaka 2020/2021 imetenga fedha kiasi cha Shilingi Milioni 20 kwa ajili ya hatua ya upimaji wa athari za kimazingira katika eneo la kidomole lililopo katika Kata ya Fukayosi kwa ajili ya kuhamisha dampo hilo toka katika eneo la Sanzale na kulihamishia eneo la kidomole.

Aidha kero za Wanachi wa Kata za Magomeni na Kata ya Dunda ambao walishiriki mikutano hiyo, zimeonekana Dhahiri kuelemea zaidi katika migogoro ya ardhi, Wanawake, wazee na watoto kutakiwa kulipia huduma za Afya wafikapo Hospitali ya Wilaya, ukosefu wa umeme katika eneo la bon’gwa, kutoboreshwa kwa Mji Mkongwe wa Bagamoyo kuwa Mji wa kisasa zaidi ili kuongeza mapato ya Serikali, uboreshwaji wa miundo mbinu ya mifereji ya maji taka katika mitaa, kutopatiwa vibali vya kufanya sherehe mbalimbali za kijamii, ukosefu wa ajira kwa vijana, Urasimu wa utoaji vitambulisho katika Ofisi za NIDA, na uchafu katika mji wa Bagamoyo, hali kadhalika, Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Zainab Kawawa alitolea ufafanuzi kero hizo zote na kuzitatua kupitia mikutano hiyo aliyofanya katika Kata hizo hapo jana.

Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Mhe Zainab Kawawa alimaliza Mikutano hiyo kwa kuwakaribisha Wananchi Ofisini kwake kila siku ya Jumanne kuanzia saa 02:00 Asubuhi hadi saa 9:30 jioni kwani siku hiyo ameitenga maalum kwa ajili ya kusikiliza kero na malalamiko ya Wananchi akishirikiana na wataalam wa Halmashauri.



Matangazo

  • TANGAZO LA KUTEULIWA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 AWAMU YA PILI... May 09, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA BAGAMOYO... February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA OBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.. February 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI... July 14, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • HALMASHAURI YA BAGAMOYO YAPANDA MITI 500 ENEO LA MNADA WA ZINGA KUBORESHA MAZINGIRA...

    April 15, 2025
  • TUTAENDELEA KUSIMAMIA KWA DHATI NA HAKI MISINGI YA DEMOKRASIA...

    April 02, 2025
  • ELIMU KUHUSU MPOX YATOLEWA KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI...

    March 20, 2025
  • WAPENI ELIMU WANANCHI KUHUSU UGOJWA WA MPOX...

    March 17, 2025
  • Angalia zote

Video

SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 0733860575

    Simu ya kiganjani: 0733860575

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo