• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Divisheni na Vitengo
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TASAF
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Usimamizi wa Usafi na Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha mawasiliano Serikalini
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2024-2025
      • Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

FANYENI KAZI KWA KUZINGATIA STK ZA UTUMISHI

Posted on: June 21st, 2019



Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Bi. Fatuma Latu amewaasa watumishi wa Halmashauri hiyo kufanya kazi kwa kuzingatia Sheria, taratibu na Kanuni (STK) za utumishi wa Umma ili kuleta matokeo chanya kwenye utumishi.

Bi. Fatuma Latu, ameyasema hayo mapema leo, wakati alipokuwa akifungua mkutano maalum wa watumishi takribani 200 wa Halmashauri hiyo, uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri, katika kilele cha maadhimisho ya juma la utumishi wa Umma.

“Kila mtumishi ahakikishe anafanya kazi kwa kuzingatia Sheria, taratibu na kanuni za utumishi wa Umma, hizi ziwe dira wakati tukitimiza majukumu yetu ya kila siku ili kuleta matokeo chanya ya utekelezaji wa shughuli za Serikali katika Halmashauri yetu” Amesema Bi. Fatuma Latu.

Bi. Fatuma Latu pia ametumia fursa hiyo kuwaasa Watumishi kuhakikisha wanajiepusha na vitendo vya rushwa, matumizi ya lugha chafu, na kuhimiza ushirikiano baina ya watumishi katika ngazi zote, huku akitanabaisha kwamba hatamvumilia mtumishi yeyote ambaye atapatikana na makosa ya kuomba ama kupokea rushwa.

Akaongeza, Suala la kutunza siri pia ni muhimu sana wakati wa utekelezaji wa Shughuli za Serikali kila mmoja katika nafasi yake, utunzaji wa Siri unatufanya kufanya kazi kwa kuaminiana na kwa usalama wakati wote hivyo kuongeza ari ya kutumikia Wananchi.

Vilevile, Mkurugenzi Mtendaji, Bi. Fatuma Latu, amewakumbusha watumishi kuhakikisha wanapata chakula bora na kujipa muda wa kupumzika baada ya kumaliza kutimiza majukumu yao ya kila siku ili mwili uwe na Afya wakati wote na kuongeza uwezo wa kufanya kazi.

Nae, Mkuu wa Idara ya Utumishi na Utawala Ndg. George Mwalukasa akizungumza na watumishi katika Mkutano huo amewahimiza watumishi kuwa makini pale wanapotakiwa kuhuisha taarifa zao za kiutumishi, kwani wengi wao wamekuwa na hulka ya kupuuzia maagizo ya usafishaji taarifa za kiutumishi yanapotolewa, kwani kupuuzia usafishaji wa taarifa za mtumishi kunaweza kupelekea mtumishi kuondolewa katika orodha ya malipo ya mshahara.

 Akaongeza, “Mtumishi ambaye hatajaza fomu za OPRAS kuaniza tarehe 01 Julai, 2019, ambapo OPRAS zitaanza kujazwa kwa njia ya kielektroniki, hatapata mshahara hadi hapo atakapokuwa amejaza fomu hiyo ya upimaji wa utendaji kazi wa Mtumishi, yaani OPRAS”.

Wakati huo huo, watumishi wamepata darasa maalum la madhara ya kujihususha na vitendo vya rushwa ambapo Afisa TAKUKURU – Elimu kwa Umma, Bi. Jane Mgaya amezungumzia mada maalum ya madhara ya vitendo vya Rushwa katika utendaji kazi wa kila mtumishi anapokuwa akitekeleza majukumu yake ya kila siku.

“Tuepuke mambo yanayopelekea uwepo wa mazingira ya vitendo vya rushwa kutengenezwa, tunapokuwa tukitekeleza majukumu yetu ya kila siku, mambo hayo ni pamoja na ukosekanaji wa uwazi katika uwajibikaji, urasimu katika utoaji huduma na tamaa ya kujipatia mafanikio kwa haraka” Amesema Bi. Jane Mgaya

Akaongeza, athari za rushwa ni kubwa kwani rushwa huondoa utu na thamani ya mtu, hudhoofisha utoaji huduma bora, kukosekana kwa uwazi na uwajibikaji katika utumishi wa umma na hupelekea mtumishi kufanya maamuzi yenye upendeleo, hivyo akasisitiza kila mmoja kushiriki katika vita dhidi ya rushwa ili kuiletea jamii yetu maendeleo kwani vita dhidi ya rushwa si ya TAKUKURU peke yake bali ni ya jamii nzima ili kuiletea jamii yetu maendeleo.

Wiki ya utumishi wa umma huadhimishwa mara moja kila Mwaka kila ifikapo Mwezi Juni, ambapo shughuli mbalimbali za kiutumishi huambatana na maadhimisho haya, ikiwa na pamoja kusikiliza kero na malalamiko toka kwa Watumishi na kuzipatia ufumbuzi, uwepo wa semina mbalimbali zinazohamasisha weledi na utawala bora katika utumishi wa umma, pamoja na mkutano maalum wa watumishi ambao hufanyika siku ya kilele cha Wiki ya Utumishi wa Umma ambao huhudhuriwa pia na wadau mbali mbali toka sekta binafsi zikiwemo taasisi za kifedha na mashirika binafsi Wilayani hapa.


Matangazo

  • TANGAZO LA KUTEULIWA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 AWAMU YA PILI... May 09, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA BAGAMOYO... February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA OBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.. February 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI... July 14, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • HALMASHAURI YA BAGAMOYO YAPANDA MITI 500 ENEO LA MNADA WA ZINGA KUBORESHA MAZINGIRA...

    April 15, 2025
  • TUTAENDELEA KUSIMAMIA KWA DHATI NA HAKI MISINGI YA DEMOKRASIA...

    April 02, 2025
  • ELIMU KUHUSU MPOX YATOLEWA KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI...

    March 20, 2025
  • WAPENI ELIMU WANANCHI KUHUSU UGOJWA WA MPOX...

    March 17, 2025
  • Angalia zote

Video

SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 0733860575

    Simu ya kiganjani: 0733860575

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo