• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Divisheni na Vitengo
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TASAF
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Usimamizi wa Usafi na Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha mawasiliano Serikalini
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2024-2025
      • Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

HALMASHAURI YA WILAYA YA BAGAMOYO YAPATA HATI SAFI KWA MIKA MITATU MFULULIZO

Posted on: July 1st, 2019

HALMASHAURI ya Wilaya ya Bagamoyo imefanikiwa kwa mara nyingine tena kupata hati safi (Unqualified Audit Opinion) kwa Mwaka wa fedha 2017/2018, ikiwa ni mara ya tatu mfululizo kwa Halmashauri ya Bagamoyo kupata hati safi.


Hayo yamesemwa leo Julai 01,2019 na Mkaguzi Mkuu Mkoa wa Pwani Bi. Mwajuma Mohamedi alipokuwa anawasilisha taarifa ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) katika kikao maalumu cha Baraza la Madiwani wa halmashauri ya Bagamoyo.


Bi. Mwajuma amelieleza baraza la Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo kuwa, kwa mujibu wa Katiba ya mwaka 1977 (Rev 2005) ibara ya 143 na sheria ya ukaguzi wa umma namba 11 ya 2918 kifungu cha 10(1) ni jukumu la la Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali kufanya ukaguzi wa taarifa za mapato na matumizi ya fedha za umma Serikali Kuu,Serikali za Mitaa,Idara na mashirika ya umma.


Akaongeza, baada ya ukaguzi huo anatakiwa kutoa matokeo ya ukaguzi na mapendekezo kutokana na ukaguzi huo na hatua zinazotakiwa kuchukuliwa na menejimenti zilizopo kwa mujibu wa sheria.


Zaidi Bi. Mwajuma anasema, "Katika ukaguzi uliofanyika kwa mwaka wa fedha 2017/2018, Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo imepata hati safi na kufanya halmashauri hii kuendelea kupata hati safi kwa miaka mitatu mfululizo, kwani kwa Mwaka 2017/2018, mwaka 2016/2017 na mwaka 2015/2016 Bagamoyo imepata hati safi ya Mkaguzi na mdhibiti Mkuu wa hesabu za Serikali (CAG)”.


Nae Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani, Bi. Theresia Mmbando akizungumza katika mkutano huo maalum wa baraza la Waheshimiwa Madiwani amesema, ni jambo la kujivunia kwa Halmashauri na Mkoa wa Pwani kwa Bagamoyo kupata hati safi kwa miaka mitatu mfululizo, na kusisitiza kwamba maelekezo na mapendekezo yaliyotolewa na Mkaaguzi na mdhibiti Mkuu wa Serikali (CAG) katika ripoti yake iliyowasilishwa katika mkutano huo, yafanyiwe kazi ili kuondoa kasoro ndogondogo zilizoonekana kipindi ukaguzi ulipofanyika, ili Halmashauri iendelee kupata hati safi miaka ijayo.


Bi. Theresia Mmbando pia ametumia fursa hiyo, kuwaasa Waheshimiwa Madiwani na Wataalam wa Halamshauri kuhakikisha wanasimamia vyema ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri na kuongeza ubunifu katika kuanzisha vyanzo vipya kwa kutilia mkazo uandishi wa maandiko ya miradi ya kimkakati inayofadhiliwa na Serikali kuu kwa sasa, itakayoisaidia Halmashauri kuongeza mapato yake ya ndani.


Akifunga Mkutano huo wa Baraza la Waheshimiwa madiwani, Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Said Ngatipura amesema, watahakikisha wanasimamia mapendekezo yote yaliyotolewa kwenye ripoti ya Mkaguzi na mdhibiti Mkuu wa Serikali na kusimamia ukusanyaji wa mapato ili kuhakikisha Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo inaendelea kufanya vizuri.


Matangazo

  • TANGAZO LA KUTEULIWA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 AWAMU YA PILI... May 09, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA BAGAMOYO... February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA OBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.. February 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI... July 14, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • HALMASHAURI YA BAGAMOYO YAPANDA MITI 500 ENEO LA MNADA WA ZINGA KUBORESHA MAZINGIRA...

    April 15, 2025
  • TUTAENDELEA KUSIMAMIA KWA DHATI NA HAKI MISINGI YA DEMOKRASIA...

    April 02, 2025
  • ELIMU KUHUSU MPOX YATOLEWA KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI...

    March 20, 2025
  • WAPENI ELIMU WANANCHI KUHUSU UGOJWA WA MPOX...

    March 17, 2025
  • Angalia zote

Video

SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 0733860575

    Simu ya kiganjani: 0733860575

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo