• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Divisheni na Vitengo
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TASAF
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Usimamizi wa Usafi na Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha mawasiliano Serikalini
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2024-2025
      • Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

HONGERENI BAGAMOYO MMEMTUA MAMA NDOO YA MAJI KICHWANI: MHE. MUSA SIMA

Posted on: March 18th, 2019

Kongole hizi zimetolewa na Naibu waziri wa ofisi ya Makamu wa Rais inayoshughulikia masuala ya Muungano na Mazingira, Mhe. Musa Sima mapema leo 

alipoiongoza Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira katika ziara maalum ya kukagua na kutembelea Miradi ya Sekta ya maji 

iliyotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo chini ya ufadhili wa Ofisi ya Makamu wa Rais kwa Mwaka wa fedha 2018/2019.

Miradi iliyotembelewa na kukaguliwa ni pamoja na ujenzi wa visima 10 vilivyojengwa na Ofisi ya Makamu wa Rais Wilayani hapa katika Kata za Kisutu,

Dunda, Magomeni, Nia njema, Zinga na Kiromo.Mradi mwingine wa Sekta ya maji uliotembelewa ni ujenzi wa Miundombinu ya Kuvunia Maji ya Mvua na 

matanki maalum 8 ya kuhifadhia maji salama ya mvua yenye uwezo wa kuhifadhi kiasi cha lita 135,000 kwa mara moja katika Shule ya Sekondari Kingani.

Ziara hiyo iliyoongozwa na Mweyekiti wa Kamati hiyo ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira, Mheshimiwa (MB) Selemani Mohamedi Sadiki Mbunge wa Mvomero

pamoja na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Muungano na Mazingira Mheshimiwa Musa Sima imeridhishwa na utekelezaji wa miradi hiyo ambayo yote hadi sasa imekamilika

na imeanza kutoa huduma kwa wanafunzi na wananchi na kuupongeza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo kupitia Idara ya maji kwa namna ilivyosimamia 

utekelezaji wa miradi hiyo kwa ubora na ufanisi mkubwa na akatumia fursa hiyo pia kutoa rai kwa Uongozi wa Halmashauri kuhakikisha unasimamia uendelevu wa miradi 

hiyo kwa kuhamasisha Wananchi kuitunza ili iwafae kwa muda mrefu.

"Nawapongeza sana kwa kuonesha thamani ya fedha katika utekelezaji wa miradi hii, Bagamoyo kwa hakika mmefanikiwa kutekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi ya kumwondolea

mama adha ya kwenda umbali mrefu akitafuta maji, Bagamoyo mmetua mama ndoo ya maji kichwani, Wananchi niwasisitize na kuwakumbusha kutunza miundombinu hii ya maji ili 

iwafae kwa muda mrefu zaidi na bodi ya maji hakikisheni mnaweka bei rafiki kwa Wananchi ambayo ni Shilingi 25 badala ya Shilingi 50 iliyopo sasa. kwa kila ndoo moja ya maji" Alisema Mheshimiwa Musa Sima

Wajumbe wa kamati hiyo wakiwa katika Shule ya Sekondari Kingani, wamepata fursa ya kusikia shuhuda mbali mbali toka kwa Wanafunzi wa Shule hiyo wakielezea namna ambavyo utekelezaji 

wa mradi huo umewanufaisha na kuwaondoa katika dhiki kubwa ya maji waliyokuwa nayo hapo awali.

Naye Mkuu wa Shule ya Sekondari Kingani Ndg. Method Kunambi amesema matanki ya maji yaliyojengwa katika Shule hiyo ambayo ni ya Bweni kwa wasichana, 

yamekuwa na faida kubwa sana kwa Wanafunzi na walimu wa Shule hiyo kwani sasa wanaweza kuokoa muda wao wa masomo, kupata maji safi na salama ya kunywa,

kusaidia katika kufundisha na kufundishia hasa masomo ya sayansi huku tatizo la magonjwa kupungua kutokana na natumizi ya maji kuwa machafu lakini pia mradi

umewasaidia kupunguza gharama za uendeshaji wa Shule katika matumizi ya Umeme na Matengenezo ya visima vya pampu.

Moja ya mradi wa visima 10, uliokaguliwa na kutembelewa ni mradi wa ujenzi wa tanki la maji lenye ujazo wa lita 4000 na vichotea maji viwili uliopo Kata ya Magomeni, 

mradi huu unaotumia umeme kujiendesha una uwezo wa kuhudumia Wananchi zaidi ya 1000 kwa siku. Kitongoji cha Bong’wa Kamati ilikagua na kujionea mradi wa mradi

wa maji unaotumia Umeme wenye uwezo wa kuhudumia Wananchi zaidi ya 500 kwa siku. Wakiwa katika eneo hilo, Mwenyekiti wa kamati, Mhe. Selemani Mohamed Sadiki 

alipongeza namna utekelezaji wa mradi huo ulivyofanyika kwa ufanisi mkubwa.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUTEULIWA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 AWAMU YA PILI... May 09, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA BAGAMOYO... February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA OBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.. February 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI... July 14, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • BAGAMOYO KUJITANGAZA KIMATAIFA SEKTA YA UTALIII...

    May 10, 2025
  • HALMASHAURI YA BAGAMOYO YAPANDA MITI 500 ENEO LA MNADA WA ZINGA KUBORESHA MAZINGIRA...

    April 15, 2025
  • TUTAENDELEA KUSIMAMIA KWA DHATI NA HAKI MISINGI YA DEMOKRASIA...

    April 02, 2025
  • ELIMU KUHUSU MPOX YATOLEWA KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI...

    March 20, 2025
  • Angalia zote

Video

SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 0733860575

    Simu ya kiganjani: 0733860575

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo