• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Divisheni na Vitengo
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TASAF
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Usimamizi wa Usafi na Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha mawasiliano Serikalini
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2024-2025
      • Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

KAMPUNI YA MAMBA CEMENT YATOA MSAADA WA VINAWIA MIKONO KWA VYUO VIKUU NA SEKONDARI ZA BAGAMOYO

Posted on: June 4th, 2020

Ikiwa ni siku tatu tu zimepita tangu Serikali kuruhusu Vyuo vikuu na Shule za Sekondari zenye wanafunzi wa kidato cha sita kufunguliwa kote Nchini, Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Zainab Kawawa, leo amepokea msaada wa matanki 22 ya maji, yenye stendi, ndoo na mabeseni ya kunawia mikono kwa ajili ya kusaidia wanafunzi hao kupata sehemu za kunawia mikono wawapo Vyuoni na Shuleni ili kuendelea kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa corona.

Akizungumza mapema leo Ofisini kwake mara baada ya kupokea msaada huo, Mhe. Zainab Kawawa amesema baada ya Serikali kutangaza kufungua Vyuo Vikuu na Shule za Sekondari zenye Wanafunzi wa kidato cha sita kote Nchini, yeye binafsi aliamua kuomba msaada huo toka kampuni ya Mamba Cement iliyopo Wilayani hapa ili kusaidia katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa corona.

“Nawashukuru sana kampuni ya Mamba cement kwa kupokea ombi langu na kutuletea msaada huu ambao ama kwa hakika umekuja kwa haraka kuliko nilivyotarajia, nawashukuru sana kwa kuona uhitaji wetu na kuleta msaada huu Wilayani Bagamoyo, kwani vinawia mikono hivi vitasaidia sana wanafunzi ambao wamerudi vyuoni na Shuleni kuendelea kujikinga dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu unaosababishwa na virusi vya Corona” Amesema Mhe. Zainab

Aidha, Mkuu wa kitengo cha Uhusiano wa Kampuni ya Mamba Cement Bw. Aboubakar Mlawa mara baada ya kukabidhi msaada huo kwa Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, amesema wao wameitika wito kwakuwa wana mahusiano mazuri na Uongozi wa Wilaya ya Bagamoyo lakini pia huu ni wakati sahihi wa kurudisha fadhila zao kwa jamii inayowazunguka kwa kushirikiana nayo katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Corona na kuongeza kuwa vinawia mikono hivyo vina thamani ya shilingi Milioni 5.500,000/-

Naye Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ukutubi na Uhifadhi nyaraka Nchini kilichopo Wilayani hapa, Bi. Victoria Kessy akizungumza kwa niaba ya Wakuu wa Vyuo na Shule za Sekondari zilizonufaika na msaada huo, msaada huo umekuja kwa wakati mwafaka na wataendelea kutoa elimu kwa wanafunzi wao kuendelea kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa Corona kwa vitendo kwa kutumia msaada wa vinawia mikono hivyo.

Baada ya Serikali kuruhusu Vyuo na Shule hizo kufunguliwa, Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo imepokea Wanafunzi katika Vyuo vikuu 8 na Shule 9 za Sekondari na Wanafunzi wanaendelea na masomo kama ilivyokuwa hapo awali.


Matangazo

  • TANGAZO LA KUTEULIWA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 AWAMU YA PILI... May 09, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA BAGAMOYO... February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA OBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.. February 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI... July 14, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • BAGAMOYO KUJITANGAZA KIMATAIFA SEKTA YA UTALIII...

    May 10, 2025
  • HALMASHAURI YA BAGAMOYO YAPANDA MITI 500 ENEO LA MNADA WA ZINGA KUBORESHA MAZINGIRA...

    April 15, 2025
  • TUTAENDELEA KUSIMAMIA KWA DHATI NA HAKI MISINGI YA DEMOKRASIA...

    April 02, 2025
  • ELIMU KUHUSU MPOX YATOLEWA KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI...

    March 20, 2025
  • Angalia zote

Video

SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 0733860575

    Simu ya kiganjani: 0733860575

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo