• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Divisheni na Vitengo
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TASAF
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Usimamizi wa Usafi na Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha mawasiliano Serikalini
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2024-2025
      • Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

KILIMO CHA MUHOGO KUKOMBOA WAKULIMA BAGAMOYO

Posted on: March 7th, 2019

KILIMO CHA MUHOGO KUKOMBOA WAKULIMA BAGAMOYO

Wakulima Wilayani Bagamoyo wamehimizwa kuongeza uzalishaji wa zao la Muhogo, kwani zao hilo kwa sasa, ni zao maalumu la kibiashara na ukombozi wa Mkulima Wilayani humo.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, mapema jana alipokuwa akizungumza na Wananchi, Waheshimiwa Madiwani na Wakuu wa Idara katika kikao maalum cha Baraza la Waheshimiwa madiwani kilichoketi kwa siku mbili, kuanzia tarehe 05 na 06 Machi, 2019.

Mhe. Mwenyekiti Alli Alli Issa ambaye pia ni diwani wa Kata ya Fukayosi ameeleza kupitia mkutano huo wa baraza la Waheshimiwa madiwani kuwa, zao la Muhogo ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo sasa ni zao la biashara na ukombozi kwa Wakulima wa Bagamoyo baada ya kuikaribisha kampuni ya Dar Canton Investment Limited ambayo ni kampuni ya Uwekezaji katika zao la muhogo inayotarajiwa kuanza kufanya kazi ndani ya Halmashauri ikijikita katika ununuzi na uchakataji wa muhogo.

“Waheshimiwa Madiwani wenzangu twende tukawahimize Wananchi kujikita katika uzalishaji wa zao mhogo bora, Wataalamu mtusaidie kufika Vijijini kuwaelimisha Wananchi juu ya kutumia mbegu bora za mhogo na kulima kilimo kinachozingatia kanuni bora za kilimo ili wapate tija katika mazao yao, na kunufaika na ujio wa mwekezaji huyu aliye tayari kununua mhogo kwa Wananchi kuanzia sasa na pale ujenzi wa kiwanda cha uchakataji mhogo utakapokamilika ni wazi Wananchi wetu watanufaika zaidi kwa kuuza mhogo kiwandani” Amesema Mhe. Alli Alli Issa.

Akizungumza katika mkutano huo, Mkurugenzi wa kampuni ya Dar Canton Investment Limited amesema kampuni imepata eneo lililopo Kata ya Makurunge, katika Kitongoji cha Kifude ambapo imeshaanza kufanya upembuzi yakinifu ili kuanza ujenzi wa kiwanda cha uchakataji wa mhogo na kwamba kwa sasa kampuni inaendelea kununua mhogo mkavu katika maeneo mbali mbali ndani ya Halmashauri na kiwanda kitakua na uwezo wa kununua tani 120 za mhogo kwa siku mara kitakapoanza uzalishaji wake, na akaongeza kuwa kwa sasa tayari wameanza ununuzi wa mhogo kwa wakulima mbalimbali ndani na nje ya Halmashauri hivyo Wananchi waendelee na uzalishaji wa mhogo kwani tayari kuna soko la uhakika kupitia kampuni yao.

Baraza la Waheshimiwa madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo limeketi kwa siku mbili kuanzia tarehe 05 na 06 machi, 2019 kujadili taarifa mbalimbali za utekelezaji za Halmashauri kwa robo ya pili kwa Mwaka wa fedha 2018/2019.



Matangazo

  • TANGAZO LA KUTEULIWA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 AWAMU YA PILI... May 09, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA BAGAMOYO... February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA OBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.. February 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI... July 14, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • BAGAMOYO KUJITANGAZA KIMATAIFA SEKTA YA UTALIII...

    May 10, 2025
  • HALMASHAURI YA BAGAMOYO YAPANDA MITI 500 ENEO LA MNADA WA ZINGA KUBORESHA MAZINGIRA...

    April 15, 2025
  • TUTAENDELEA KUSIMAMIA KWA DHATI NA HAKI MISINGI YA DEMOKRASIA...

    April 02, 2025
  • ELIMU KUHUSU MPOX YATOLEWA KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI...

    March 20, 2025
  • Angalia zote

Video

SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 0733860575

    Simu ya kiganjani: 0733860575

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo