• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Divisheni na Vitengo
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TASAF
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Usimamizi wa Usafi na Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha mawasiliano Serikalini
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2024-2025
      • Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

KLABU ZA HAKI ZA BINADAMU KUANZISHWA MASHULENI

Posted on: November 9th, 2020

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), katika kutekeleza majukumu yake ya kuijengea jamii uwezo wa kuzifahamu Haki na Wajibu wa Jamii juu ya Haki hizo, kimeanzisha programu maalum ya kuifikia jamii kwa haraka zaidi kupitia kundi la watoto na Vijana ambao watapatiwa mafunzo maalumu juu ya Haki za Binadamu hususani Haki za Watoto.

DSC_0151.JPG

Kundi hili la Watoto na Vijana linaaminika kuwa kundi muhimu hasa kwa namna ambavyo wakipatiwa elimu juu ya Haki za Binadamu linaweza kusambaza elimu hiyo kwa jamii nzima kwa haraka zaidi kwa kuibeba elimu hiyo na kuifikisha kwa makundi mengine yanayowazunguka katika jamii kama wazazi, walezi na kila mwanajamii aliye na uhusiano na kundi hili la Watoto na Vijana.

Katika kufanikisha hili Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimeweka kambi Wilayani Bagamoyo ili kuendesha mafunzo maalumu ya siku 03 kwa Maafisa elimu Kata wa Kata zote 11 za Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo na Maafisa Ustawi wa Jamii wanaoshughulikia dawati la marekebisho ya Tabia na Haki za Mtoto Kisheria, mafunzo yanayolenga kuwajengea uwezo Wataalamu hao wa Halmashauri kusimamia uendeshaji wa Klabu zote za Haki za Binadamu zilizoanzishwa Mashuleni katika Kila Shule ya Msingi na Sekondari katika Kata zote 11 za Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo.

Akifungua mafunzo hayo maalumu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo Bi. Fatuma O. Latu, ameshukuru Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kufikiria kuanzisha Klabu hizo Mashuleni kwani ni Klabu hizo zitakuwa msaada mkubwa kwa wanafunzi hao kupata uelewa wa namna ya kujilinda dhidi ya vitendo vya ukatili na wajibu wao katika kusimamia haki zao.

DSC_0184.JPG

“Tunaahidi kushirikiana nanyi katika program hii ili kwa pamoja tuweze kuwasaidia watoto wetu kuzifahamu Haki zao za Msingi hii itawasaidia sana kujilinda dhidi ya vitendo vya ukatili na sisi kama Halmashauri tutaiweka shughuli hii katika mpango na bajeti wa Halmashauri ili kuongeza nguvu na kuhakikisha programu hii inafanikiwa kuwakomboa Watoto na Vijana wetu waliopo Mashuleni na majumbani dhidi ya vitendo vya Ukatili na kujenga Taifa imara na jamii yenye uelewa juu ya Haki za Binadamu.

Klabu za Haki za Binadamu (Haki za Watoto) zitaanzishwa katika Shule zote 77 za Msingi na Sekondari za Serikali na binafsi Wilayani Bagamoyo baada ya kuonekana uhitaji mkubwa wa uanzishwaji wa Klabu hizo kutokana na kukithiri kwa vitendo vya ukatili dhidi ya watoto, hususani kuongezeka kwa vitendo vya ubakaji, ulawiti na mimba za utotoni.

Ndg. Ally Seif Ramadhani ni Mratibu wa Programu ya Vilabu vya Haki za Binadamu na Vijana kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu anaeleza malengo ya program hii kuwa ni kuwajengea uwezo wanafunzi juu ya Haki za Binadamu hususani Haki za Watoto na wajibu ili kuepukana na vitendo vya ukatili na namna ya kutoa taarifa mahala panapohusika pale wanapofanyiwa vitendo vya Ukatili.

Wakati huo huo Mratibu wa Dawati la Marekebisho ya tabia na Haki za Mtoto Kisheria Wilaya ya Bagamoyo Bi. Flora Warioba amesisitiza juu ya umuhimu wa uanzishwaji wa klabu za Haki za Binadamu (Haki za Mtoto) Mashuleni kwani zitakuwa kitovu cha kukomesha vitendo vya ukali dhidi ya watoto na Vijana Wilayani Bagamoyo na kuahidi kusimamia program hiyo kikamilifu ili ilete mafanikio yanayotarajiwa katika jamii ya Wana Bagamoyo.


Matangazo

  • TANGAZO LA KUTEULIWA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 AWAMU YA PILI... May 09, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA BAGAMOYO... February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA OBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.. February 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI... July 14, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • HALMASHAURI YA BAGAMOYO YAPANDA MITI 500 ENEO LA MNADA WA ZINGA KUBORESHA MAZINGIRA...

    April 15, 2025
  • TUTAENDELEA KUSIMAMIA KWA DHATI NA HAKI MISINGI YA DEMOKRASIA...

    April 02, 2025
  • ELIMU KUHUSU MPOX YATOLEWA KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI...

    March 20, 2025
  • WAPENI ELIMU WANANCHI KUHUSU UGOJWA WA MPOX...

    March 17, 2025
  • Angalia zote

Video

SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 0733860575

    Simu ya kiganjani: 0733860575

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo