• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Divisheni na Vitengo
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TASAF
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Usimamizi wa Usafi na Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha mawasiliano Serikalini
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2024-2025
      • Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

TEMESA USO KWA USO NA WATAALAM WA HALMASHAURI YA BAGAMOYO

Posted on: September 22nd, 2020

Wakuu wa Idara na vitengo wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo leo Septemba 22, 2020, wamefanya kikao maalum na wataalam kutoka Wakala wa ufundi na Umeme (TEMESA) Mkoa wa Pwani ili kujadiliana changamoto mbalimbali zinazotokea pale Halmashauri inapohitaji huduma za utengenezaji wa magari toka kwa wakala hao na kujadili namna bora ya ufumbuzi wa changamoto hizo kwa pamoja.


Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Bi. Fatuma O. Latu, aliyeongoza kikao hicho amesema, imekuwa vyema kuketi katika meza moja kujadili changamoto hizo badala ya utaratibu wa barua ambao wamekua wakiutumia mara zote.
“Tunashukuru mmekubali wito wetu wa kufika hapa ili tutafute ufumbuzi wa changamoto tunazokumbana nazo wakati Halmashauri inapohitaji huduma za kutengenezewa magari toka TEMESA, ambapo changamoto kubwa imekuwa ni ucheleweshwaji wa kumalizika kwa kazi, ubora wa vipuri, gharama za vipuri na gharama kubwa za utengenezaji wa magari, tunaamini kikao hiki kitakuwa ni msaada mkubwa kwetu na kitasaidia kupata ufafanuzi wa changamoto hizi na tutazipatia ufumbuzi wa pamoja ili na sisi kama Halmashauri tuendelee kutoa huduma kwa Wananchi kwa wakati hasa pale itakapotuhitaji kutumia magari kutoa huduma hizo” Amesema Mkurugenzi Fatuma.

Nae Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mkoa wa Pwani, Mhandisi Rehema Juma akizungumza katika mkutano huo ameshukuru uongozi wa Halmashashuri ya Wilaya ya Bagamoyo, kuona umuhimu wa kukaa meza moja ili kujadiliana na kuzitafutia ufumbuzi wa pamoja changamoto zinazojitokeza katika utendaji kazi wa TEMESA wakati wa kutoa huduma hasa za utengenezaji magari ya Halmashauri huku akikiri kuwa TEMESA bado ina mapungufu katika utoaji huduma kwani na wao wanakabiliana na changamoto kadha wa kadha ikiwa ni pamoja ana ucheleweshwaji wa malipo toka kwa taasisi wanazozihudumia, ubora wa vipuri, gharama za vipuri, upungufu wa Watumishi, na kupongeza hatua ya Serikali kuhakikisha vipuri vyote vya magari vitakavyofungwa katika magari kuanzia sasa kuwa vimethibitishwa na TBS, hivyo mamlaka hiyo ya udhibiti ubora kuanzia sasa itakuwa ikifanya kazi bega kwa bega na TEMESA ili kuhakikisha ubora wa vipuri vitakavyofungwa katika magari ya Serikali.

Mhandisi Rehema, pia ametumia fursa hiyo kumwomba Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo kumalizia madeni ya utengenezaji magari ambayo bado hayajalipwa TEMESA yanayokaribia Shilingi Milioni 27 katika kipindi cha Mwaka 2017 – 2020 ili Taasisi hiyo iweze kutumia fedha hizo katika uboreshaji wa utoaji huduma zake kwa taasisi zingine za Serikali katika Mkoa wa Pwani.

Mkutano huo umekamilika kwa pande zote mbili kuahidiana ushirikiano katika kutekeleza majukumu ya Serikali ili kurahisisha utoaji huduma kwa wananchi kwa haraka na kwa weledi huku Mkurugenzi Fatuma akiahidi kuweka mkakati maalum wa kumaliza deni hilo haraka iwezekanavyo.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUTEULIWA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 AWAMU YA PILI... May 09, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA BAGAMOYO... February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA OBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.. February 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI... July 14, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • HALMASHAURI YA BAGAMOYO YAPANDA MITI 500 ENEO LA MNADA WA ZINGA KUBORESHA MAZINGIRA...

    April 15, 2025
  • TUTAENDELEA KUSIMAMIA KWA DHATI NA HAKI MISINGI YA DEMOKRASIA...

    April 02, 2025
  • ELIMU KUHUSU MPOX YATOLEWA KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI...

    March 20, 2025
  • WAPENI ELIMU WANANCHI KUHUSU UGOJWA WA MPOX...

    March 17, 2025
  • Angalia zote

Video

SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 0733860575

    Simu ya kiganjani: 0733860575

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo