• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Divisheni na Vitengo
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TASAF
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Usimamizi wa Usafi na Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha mawasiliano Serikalini
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2024-2025
      • Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

TUTADHIBITI MIANYA YOTE YA UPOTEVU WA MAPATO: MPWIMBWI

Posted on: September 16th, 2020


Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mji mdogo Bagamoyo, Mhe. Amiri Mpwimbwi ameyasema hayo leo Septemba 16, 2020 katika mkutano maalum wa baraza la Mji mdogo, uliofanyika katika Ukumbi wa TasuBa Wilayani hapa.

Akiutambulisha mkakati maalum wa Wenyeviti wa mamlaka hiyo waliojiwekea kuhakikisha wanadhibiti mianya yote ya upotevu wa mapato katika maeneo wanayoyasimamia kiuongozi, Mhe. Mpwimbwi amesema kuanzia sasa wamejiwekea mkakati maalum wa kufanya doria kubaini wafanyabiashara wasio waaminifu wanaokwepa kutoa ushuru wa Halmashauri hasa katika maeneo ya uchimbaji mchanga na mnada mkubwa wa samaki katika Pwani ya Bagamoyo Kata ya Dunda.

“Tumeamua na tutahakikisha tunashirikiana kikamilifu na Mkurugenzi Mtendaji kupitia kikosi kazi maalum cha ufuatiliaji mapato ya Halmashauri kuhakikisha wale wote wanaotukwamisha kukusanya mapato kwa usahihi katika vyanzo vya machimbo ya mchanga na mnada wa samaki Dunda tunawabaini na kuhakikisha wanachukuliwa hatua stahiki ili kupandisha ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri yetu ya Bagamoyo kwa maendeleo ya wana Bagamoyo wote” Amesema Mhe. Mpwimbwi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo kupitia mkutano huo, amewataka Wenyeviti hao kuendelea kumuunga mkono katika suala la ukusanyaji mapato katika maeneo yao na kuhakikisha wakati wote wanatoa ushirikiano katika miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali katika ameneo yao kwa kuisimamia  na kushiriki katika kamati za ujenzi wa miradi hiyo inayotekelezwa kwa utaratibu wa ‘force Account’ almaarufu kama Local fundi, ili miradi hiyo ilete tija inayotarajiwa na Serikali katika maeneo yao.

Baraza la Mji mdogo (Bagamoyo) likiongozwa na Mwenyekiti wake Amiri Mpwimbwi, mbali ya kujadili masuala ya ukusanyaji mapato pia limepokea taarifa mbali mbali za utekelezaji wa shughuli za Halmashauri.

Wenyeviti takribani 140 wamepokea taarifa ya mrejesho wa mpango wa bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka wa fedha 2020-2021 mapato ya ndani baada ya kupitishwa na bunge.

Taarifa nyingine iliyopkelewa katika mkutano huo wa baraza ni taarifa ya mchanganuo wa fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa Mwaka wa fedha 2020/2021 na taarifa ya mgao wa fedha za EP4R awamu ya nane 2019-2020.


Matangazo

  • TANGAZO LA KUTEULIWA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 AWAMU YA PILI... May 09, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA BAGAMOYO... February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA OBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.. February 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI... July 14, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • BAGAMOYO KUJITANGAZA KIMATAIFA SEKTA YA UTALIII...

    May 10, 2025
  • HALMASHAURI YA BAGAMOYO YAPANDA MITI 500 ENEO LA MNADA WA ZINGA KUBORESHA MAZINGIRA...

    April 15, 2025
  • TUTAENDELEA KUSIMAMIA KWA DHATI NA HAKI MISINGI YA DEMOKRASIA...

    April 02, 2025
  • ELIMU KUHUSU MPOX YATOLEWA KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI...

    March 20, 2025
  • Angalia zote

Video

SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 0733860575

    Simu ya kiganjani: 0733860575

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo