• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Divisheni na Vitengo
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TASAF
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Usimamizi wa Usafi na Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha mawasiliano Serikalini
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2024-2025
      • Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

UJAZAJI WA OPRAS NI LAZIMA KWA MTUMISHI WA UMMA

Posted on: August 13th, 2019


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo Bi. Fatuma O. Latu, ametoa wiki moja kwa watumishi wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo kuhakikisha wamekamilisha ujazaji wa fomu ya tathmini ya utendaji wa watumishi wa umma yaani OPRAS.

Hayp yamesemwa leo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Bi. Fatuma O. Latu, katika kikao maalum cha watumishi kinavyofanyika mara moja kwa kila robo kikiwa na lengo la kuwakumbusha watumishi majukumu yao, kuhimiza uwajibikaji na uadilifu katika utumishi, pia kusikiliza kero, malalamiko na changamoto za watumishi na kuzipatia ufumbuzi.

“Kila Mtumishi ahakikishe amejaza fomu ya upimaji wa utendaji kazi yaani OPRAS kwani ndio kipimo pekee kinachotusaidia kujua malengo yako ya kiutumishi na namna ulivyoyatekeleza kwa kuzingatia bajeti ya Halmashauri, mpango mkakati wa Halmashauri na utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi, maagizo ya viongozi na shughuli za Kitaifa. Fomu zote za OPRAS zijazwe kikamilifu na kuwasilishwa kwa Wakuu wa Idara husika, na akasisitiza kwamba mtumishi ambaye hatajaza fomu hiyo ya Upimaji yaani OPRAS, hatakuwa na majukumu ya kiutumishi ya kutekeleza kwa Mwaka husika na mtumishi asiye na majukumu ya kutekeleza hastahili kuendelea kuwa mtumishi wa umma” Amesema Bi. Fatuma Latu.

Nae Mkuu wa Idara ya Utumishi na Utawala Ndg. George Mwalukasa, akizungumza katika kikao hicho amesisitiza kuwa ili kuendelea kutekeleza majukumu ya kiutumishi katika utumishi wa umma, ni lazima utendaji wa kila mtumishi uweze kupimwa kwa kujua mtumishi ametekeleza majukumu yapi katika mwaka husika, na kuongeza kwamba watumishi ambao hawatajaza fomu hizo kwa mwaka husika wataondolewa katika orodha ya malipo ya watumishi yaani ‘payroll’ hadi hapo watakapojaza fomu hizo.

Watumishi takribani 180 waliohudhuria kikao hicho zaidi ya kupata maelekezo ya kiutendaji katika utumishi wa umma, pia walipata fursa ya kuwasilisha kero na changamoto wanazokumbana nazo katika utumishi, huku wengi wakilalamikia ucheleweshwaji wa stahili za kiutumishi kama pesa za kujikimu baada ya kuajiriwa, kubadilishiwa mishahara baada ya kupandishwa madaraja na malipo ya saa za ziada kazini, malalamiko ambayo yalitolewa ufafanuzi na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri  na kuahidi kusimamia ulipwaji wa stahili zote za watumishi zilizo halali kulingana na upatikanaji wa fedha.



Matangazo

  • TANGAZO LA KUTEULIWA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 AWAMU YA PILI... May 09, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA BAGAMOYO... February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA OBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.. February 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI... July 14, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • HALMASHAURI YA BAGAMOYO YAPANDA MITI 500 ENEO LA MNADA WA ZINGA KUBORESHA MAZINGIRA...

    April 15, 2025
  • TUTAENDELEA KUSIMAMIA KWA DHATI NA HAKI MISINGI YA DEMOKRASIA...

    April 02, 2025
  • ELIMU KUHUSU MPOX YATOLEWA KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI...

    March 20, 2025
  • WAPENI ELIMU WANANCHI KUHUSU UGOJWA WA MPOX...

    March 17, 2025
  • Angalia zote

Video

SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 0733860575

    Simu ya kiganjani: 0733860575

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo