• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Divisheni na Vitengo
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TASAF
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Usimamizi wa Usafi na Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha mawasiliano Serikalini
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2024-2025
      • Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

UTENGAJI WA ASILIMIA 5 ZA FEDHA ZA WANAWAKE NI LAZIMA - RC NDIKILO

Posted on: March 9th, 2019



Mkuu wa Mkoa wa Pwani  Mhe. Eng. Evarist Ndikilo ameziagiza Halmashauri zote za mkoa huo kuhakikisha zinatenga asilimia tano ya mapato yao ya ndani kwa ajili ya mfuko wa maendeleo ya wanawawake.

Agizo hilo lilitolewa kwa niaba yake na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Mhe. Assumpta Mshama kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika kimkoa katika Uwanja wa Saba saba, Picha ya Ndege Kibaha ambapo Mhe. Eng. Evarist Ndikilo alitarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo.

Akizungumza katika maadhimisho hayo, Mhe. Assumpta amesema ni Wakurugenzi wa Halmashauri 4 tu kati ya 9 za Mkoa wa Pwani ndizo ambazo zimetekeleza agizo la utengaji wa asilimia 5 ya mapato ya ndani kwa ajili ya mfuko wa Wanawake na kuzikabidhi fedha hizo kwa vikundi vya Wanawake kwa wakati, kama ilivyoelekezwa na Serikali.

“Wakurugenzi wa Halmashauri, nawaagiza kuwa ni lazima fedha hizi za mfuko wa Wanawake zitengwe na zitolewe kwa wakati na ziwafikie walengwa ili waweze kujiendeleza katika shughuli zao mbalimbali za kiuchumi wanazozifanya na maofisa mnaohusika na ufuatiliaji wa Wanawake hawa, muhakikishe mnazifuatilia fedha hizi kwa ukaribu ili kuona kama zinafanya kazi iliyokusudiwa na wahakikishe wanazifuatilia pia marejesho yake ili ziweze kuwasaida Wanawake wengine” Amesema Mhe. Assumpta.

Alisema katika kuwawezesha wanawake kiuchumi, ni wajibu wa kila Halmashauri kuhakikisha inaandaa na kuendesha mafunzo maalum ya ujasiriamali kwa Wanawake, lengo likiwa ni kuwajengea uwezo katika shughuli zao za kijasiriamali hususani katika usindikaji, ufungaji na masoko ya bidhaa wanazozitengeneza, ili waweze kukua na kuuza bidhaa zao ndani na nje ya Nchii, hii itawasaidia kuwawezesha wanawake kushiriki katika kuleta mabadiliko ya kiuchumi kuanzia ngazi ya familia na Taifa kwa ujumla.

Mhe. Assumpta pia ametumia fursa hiyo kuihamasisha jamii juu ya mambo ya usawa wa kijinsia,kwa kupinga ukatili wa kijinsia, na kuiasa jamii kuwa kila mmoja ashiriki katika vita ya ukatili dhidi ya wanawake na mimba za utotoni.

Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani kwa Mwaka huu 2019, yamebebwa na Kauli mbiu inayosema “badili fikra kufikia usawa wa kijinsia kwa maendeleo endelevu” hivyo Mhe. Assumpta akatumia kauli mbiu hiyo pia kuwaasa wazazi, walezi na Wanafunzi wa kike kubadili fikra juu ya umuhimu wa elimu, na kuipa elimu kipaumbele kwa kuhakikisha Wanafunzi wote waliojiunga na masomo hawaachi shule, wanaendelea na masomo ili kujenga taifa lililoelimika baadae.




Matangazo

  • TANGAZO LA KUTEULIWA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 AWAMU YA PILI... May 09, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA BAGAMOYO... February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA OBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.. February 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI... July 14, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • BAGAMOYO KUJITANGAZA KIMATAIFA SEKTA YA UTALIII...

    May 10, 2025
  • HALMASHAURI YA BAGAMOYO YAPANDA MITI 500 ENEO LA MNADA WA ZINGA KUBORESHA MAZINGIRA...

    April 15, 2025
  • TUTAENDELEA KUSIMAMIA KWA DHATI NA HAKI MISINGI YA DEMOKRASIA...

    April 02, 2025
  • ELIMU KUHUSU MPOX YATOLEWA KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI...

    March 20, 2025
  • Angalia zote

Video

SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 0733860575

    Simu ya kiganjani: 0733860575

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo