• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Divisheni na Vitengo
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TASAF
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Usimamizi wa Usafi na Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha mawasiliano Serikalini
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2024-2025
      • Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

WANAFUNZI 320 MAPINGA WAPATIWA MAJI SAFI NA SALAMA

Posted on: March 23rd, 2020


Jumla ya Wanafunzi 320 ya Shule ya Sekondari ya Kata ya Mapinga wameondokana na kero ya ukosefu wa maji baada ya taasisi ya It’s time to help foundation Tanzania ikishirikiana na Feza Schools Tanzania kutekeleza mradi wa uchimbaji kisima katika Shule hiyo ambayo haikuwa na huduma ya maji tangu kuanzishwa kwake.

Hafla ya makabidhiano ya mradi huo imefanyika Shuleni hapo siku ya tarehe 23/03/2020 baada ya mradi huo uliogharimu jumla ya Shilingi Milioni 12, kukamilika hivyo kisima hicho kukabidhiwa rasmi kwa Uongozi wa Shule hiyo ili kianze kutumika.

Afisa Uhusiano wa Taasisi ya It’s time to help Tanzania, Ndg. Mbwana Kitendo akizungumza kwenye makabidhiano ya mradi huo amesema, taasisi hiyo ina utaratibu wa kutoa misaada kwa jamii katika sekta za Afya, elimu na Sekta ya ustawi wa jamii ambapo pia hutoa misaada kwa vituo vinavyohudumia watoto wanaotoka katika mazingira magumu.

“Ni kiu yetu kuona tunaipunguzia jamii baadhi ya changamoto hasa zinazowakabili watoto katika kujenga Taifa la kesho imara, baada ya kupata taarifa kuwa wanafunzi takribani 320 wa Shule hii mpya ya Sekondari wana changamoto kubwa ya ukosefu wa maji, tuliona umuhimu wa kuja kuwasaidia kupata huduma ya maji hasa ikizingatiwa kuwa maji ni uhai na ni uhitaji muhimu kwa mwanadamu yeyote. Kutatua changamoto hii kwetu ni mafanikio makubwa kwani tunaamini sasa wanafunzi watasoma kwa amani bila kufikiri tena changamoto ya kukosa maji na hii itawaongezea utulivu na ubunifu katika masomo yao” Amesema Bw. Mbwana

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo Bw. Julius Mwanganda ameishukuru taasisi ya hiyo kwa kuona uhitaji uliokuwepo Shuleni hapo na kuwa tayari kutoa msaada huo adhimu kwani ni ukweli usiopingika kuwa Shule hiyo ilikuwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa maji, hali iliyowaletea usumbufu mkubwa na kuwaondolea utulivu wanafunzi hasa wa kike na si wanafunzi tu hata walimu kwani maji ni huduma muhimu na ya msingi kwa mwanadamu yeyote mahali popote, hivyo utatuzi wa changamoto hii utaleta ufanisi mkubwa kielimu na utendaji kazi kwa ujumla shuleni hapo.


Kwa upande wake Mkuu wa shule ya sekondari Mapinga, Bi. Agnes Mmbaga amesema awali walikuwa wakitumia maji toka katika kisima cha kuchimba kwa mkono kilichochimbwa na walimu pembezoni mwa Shule hiyo, ambacho hakikuwa na maji ya uhakika wala salama kiafya, hali hii ilipelekea kupoteza muda mwingi kutafuta maji badala ya kutumia muda huo kwenye masomo, hivyo mradi huo wa maji ni ukombozi kwa wanafunzi na walimu wa Shule hiyo huku akiahidi kuutunza mradi huo ili uendelee kutoa huduma hiyo muhimu kwa muda mrefu.


Bi. Mmbaga anaongeza, “Shule yetu hii ni mpya ndio imeanza kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza Mwezi Januari Mwaka huu, na kwa hakika bado ina chanagmoto nyingi ikiwemo upungufu wa vyumba vya madarasa, uzio, umeme, maabara, maktaba, matundu ya vyoo na Ofisi ya Walimu, hivyo nawaomba wadau wa elimu kufika katika Shule yetu na kutusaidia kutatua changamoto hizi ili kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia hali itakayoinua kiwango cha taaluma Shuleni hapo” Amesema Bi. Mmbaga.


Shule mpya ya Sekondari Mapinga, ni Shule Mpya ya Kata katika Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo. Shule hii ilianza kujengwa mapema mwaka 2019 kwa nguvu za wananchi, Halmashauri na wadau wa maendeleo katika Kata hiyo na ilipata usajili Mwezi Januari mwaka huu ambapo baada ya usajili huo ilianza kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza kutoka katika Vitongoji vya Kata ya Mapinga na imekuwa msaada mkubwa kwa wanafunzi wa Kata hiyo ambao hapo awali walilazimika kutembea umbali mrefu kwenda kupata elimu ya Sekondari katika Shule za kata za jirani za Kerege na Kiromo.







Matangazo

  • TANGAZO LA KUTEULIWA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 AWAMU YA PILI... May 09, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA BAGAMOYO... February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA OBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.. February 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI... July 14, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • BAGAMOYO KUJITANGAZA KIMATAIFA SEKTA YA UTALIII...

    May 10, 2025
  • HALMASHAURI YA BAGAMOYO YAPANDA MITI 500 ENEO LA MNADA WA ZINGA KUBORESHA MAZINGIRA...

    April 15, 2025
  • TUTAENDELEA KUSIMAMIA KWA DHATI NA HAKI MISINGI YA DEMOKRASIA...

    April 02, 2025
  • ELIMU KUHUSU MPOX YATOLEWA KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI...

    March 20, 2025
  • Angalia zote

Video

SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 0733860575

    Simu ya kiganjani: 0733860575

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo