• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Divisheni na Vitengo
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TASAF
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Usimamizi wa Usafi na Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha mawasiliano Serikalini
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2024-2025
      • Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

WANANCHI BAGAMOYO WAHAMASISHWA KUFANYA USAFI WA MAZINGIRA KILA SIKU

Posted on: January 28th, 2019

Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, hususani Wananchi wa Kata ya Dunda na Magomeni wamehamasishwa juu ya kujenga mazoea ya kufanya usafi wa mazingira yanayowazunguka mara kwa mara bila kungoja jumamosi ya mwisho wa mwezi ya usafi kama wanavyofanya sasa.

Uhamasishaji huo umefanyika siku ya jumamosi ya tarehe 26 Januari, 2019 kupitia kongamano maalum la usafi wa mazingira lililofanyika katika Soko la Magomeni lililopo Kata ya Nia njema na kuhudhuriwa na Wananchi takribani 200 wa Kata Magomeni na Kata jirani za Dunda, Kisutu na Nia njema.

Kongamano hilo limefanyika chini ya udhamini wa shirika liitwalo CVM (Communita Volontari per il Mondo) Shirika lisilo la Kiserikali linalotekeleza miradi ya maendeleo ya jamii Nchini Tanzania. Shirika la CVM Wilayani Bagamoyo linatekeleza mradi uitwao vijana ni Taifa la kesho wenye lengo la kuboresha fursa za kiuchumi na kazi kwa vijana, kukuza upatikanaji wa elimu kwa Wasichana walio katika mazingira magumu zaidi pamoja na kukuza ufahamu miongoni mwa vijana kuhusu masuala ya vijana na jinsia.

Akizungumza na Wananchi waliojitokeza kwenye kongamano hilo, Kaimu Mkuu wa Idara ya Usafi na mazingira wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo Bw. Moses Mgalla amesema usafi wa mazingira ni jukumu la msingi kila Mwananchi, kwani usafi ni Afya.

“Niwahamasishe Wananchi wote wa Bagamoyo kuona kuwa usafi ni jukumu la msingi, kila mwananchi ahamasike na ajenge tabia ya kufanya usafi wa mazingira yanayomzunguka kila siku hasa kipindi hiki tunachoelekea mvua za masika ambapo nyasi huota kwa wingi kuzunguka makazi yetu, majani hayo yafyekwe ama kulimwa na mazingira yanayotuzunguka yawe safi wakati wote” Amesema Bw. Mgalla.

Anaongeza kusema kuwa katika zama hizi za sasa ni aibu kwa Mwananchi awaye yeyote kutokuwa na choo bora, hivyo akatumia fursa hiyo kuwahamasisha Wananchi juu ya ujenzi wa vyoo bora vya gharama nafuu na kueleza kwamba choo kisicho salama kwa matumizi ya Binadamu ni hatari kwa afya ya mtumiaji na jamii kwa ujumla na kuwaasa Wananchi kuhakikisha wananawa mikono kwa kutumia sabuni kila mara wanapotoka chooni na kabla ya kula.

Naye Mwenyekiti wa Serikali ya Kitongoji cha Magomeni B, Bw. Mwinyi VuguVugu Hamidu amelishukuru shirika la CVM na Wataalam wa Usafi wa mazingira toka Halmashauri kwa kuitembelea Kata ya Magomeni na kuwapatia elimu hiyo ya usafi wa mazingira ambayo itawafaa sana, ili waishi katika mazingira safi siku zote na kuepukana na magonjwa ya mlipuko yanayosababishwa na kuishi kwenye mazingira machafu.

Wakati huo huo, Usafi wa mazingira unaofanyika kila jumamosi ya mwisho wa mwezi, umefanyika kwa ufanisi katika Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo huku maeneo mengi yakionekana safi mara baada ya kukamilika kwa usafi huo, zoezi lililoonesha mwitikio mkubwa toka kwa Wananchi na jamii ya Wanabagamoyo kwa ujumla.


Matangazo

  • TANGAZO LA KUTEULIWA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 AWAMU YA PILI... May 09, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA BAGAMOYO... February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA OBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.. February 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI... July 14, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • HALMASHAURI YA BAGAMOYO YAPANDA MITI 500 ENEO LA MNADA WA ZINGA KUBORESHA MAZINGIRA...

    April 15, 2025
  • TUTAENDELEA KUSIMAMIA KWA DHATI NA HAKI MISINGI YA DEMOKRASIA...

    April 02, 2025
  • ELIMU KUHUSU MPOX YATOLEWA KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI...

    March 20, 2025
  • WAPENI ELIMU WANANCHI KUHUSU UGOJWA WA MPOX...

    March 17, 2025
  • Angalia zote

Video

SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 0733860575

    Simu ya kiganjani: 0733860575

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo