• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Divisheni na Vitengo
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TASAF
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Usimamizi wa Usafi na Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha mawasiliano Serikalini
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2024-2025
      • Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

WARAIBU WA DAWA ZA KULEVYA KUANZA KUPATIWA MATIBABU KATIKA HOSPITALI YA WILAYA BAGAMOYO

Posted on: December 13th, 2019


Waraibu wa madawa ya kulevya katika Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, wataanza kupatiwa matibabu bure yatakayowasaidia kuachana na matumizi ya dawa za kulevya, matibabu yanayotambulika kama methadone

Matibabu haya yataanza kutolewa rasmi kuanzia tarehe 16/12/2019, saa 11:00 Alfajiri katika jengo jipya la kliniki ya methadone lililojengwa ndani ya Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo na yatatolewa bure kwa waraibu walioathirika na matumizi ya dawa za kulevya walio tayari kuachana na matumizi ya dawa za hizo.


Kuelekea kuanza utoaji wa huduma hii mnamo tarehe 16/12/2019, Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Zainab Kawawa amefanya uhamasishaji maalum kwa waraibu na jamii nzima ya wakazi wa Bagamoyo, uhamasishaji ambao umefanyika siku ya tarehe 12/12/2019, kwa kufanya mkutano katika eneo la pwani (beach) zilipokuwa Ofisi za Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), eneo hilo hukaliwa zaidi na vijana walioathirika na matumizi ya madawa ya kulevya, ambapo Mhe. Mkuu wa Wilaya ametumia fursa hiyo kuzungumza nao na kuwapa hamasa ya kwenda kupatiwa matibabu ya methadone kwenye kliniki mpya ya methadone katika Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo.

“Tumekuja na mpango mzuri wa Serikali wa kuwanusuru toka katika matumizi ya dawa za kulevya, tumefanya juhudi kubwa kutafuta wadau na kuwaomba watusaidie kupata kliniki hii ya methadone katika Wilaya yetu ambayo ina waathirika wengi vijana wa dawa za kulevya, na nina Imani mtaitumia fursa hii kuhamasishana wenyewe kwa wenyewe kwenda kupata matibabu ya methadone yatakayowasaidia kuondokana na matumizi ya dawa za kulevya, na kujirejeshea heshima na uaminifu mlioupoteza katika jamii” Amesema Mhe. Zainab Kawawa

Ameongeza, Vijana ni nguvu kazi ya Taifa, nguvu kazi hii inapopotea kwa vijana kujihusisha na matumizi ya dawa za kulevya, Taifa linachelewa kupiga hatua za maendeleo, jitokezeni kwa wingi katika kliniki hii ili mpatiwe matibabu ili mrejee kuwa vijana wenye utashi, akili timamu na wenye nguvu, kwani Taifa linawategemea na tunahitaji jamii huru na salama, ambayo tutashirikiana kwa pamoja kuiletea Nchi yetu maendeleo na niwatie moyo kuwa inawezekana kabisa kuachana na matumizi ya dawa za kulevya.

Dr. Eric Aris ni Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Kimarekani la MDH (Management and Development for Health) lililofadhili ujenzi wa kiliniki ya methadone katika Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, ametumia fursa hiyo kuwahamsisha Vijana kuhakikisha wanaitumia kliniki ya methadone kwa tija kwa kuweka nia ya kuchukia kuwa mwathirika wa dawa za kulevya na kuamua kuacha kwa kuanza matibabu ya methadone

Mmoja wa waraibu aliyepata matibabu ya methadone na kupona kutoka Kata ya Zinga, Bw. Rashid Abdallah (35), akitoa ushuhuda wake katika hadhira hiyo amesema, aliingia katika matumizi ya dawa za kulevya kwa kushawishiwa na kijana mwenzake wakati akifanya kazi za ukondakta wa daladala jijini Dar Es Salaam, huku mwenzake huyo akiwa ni dereva wa dala dala aliyokuwa akifanyia kazi

Anaongeza kusema, Nilipoteza heshima na uaminifu kwa jamii yangu hasa ndugu zangu kwa kuwa matumizi ya dawa za kulevya yalinipelekea kuwa mwizi kila nilipoingia nilihakikisha natoka na kitu ambacho ningekiuza kujipatia fedha za kununulia dawa za kulevya, jamii yangu ilinitenga na kuninyanyapaa, na nilipochoshwa na hali hiyo, niliamua kuanza matibabu ya methadone katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, nilikuwa natoka Zinga kwenda Muhimbili kila siku kufuata matibabu ya methadone, na hii ilikuwa gharama kubwa kwangu.

“Wazazi wa Vijana wa Bagamoyo shirikianeni na Vijana wenu, watienu moyo na wahamasisheni kwenda kupata matibabu ya methadone ili waondokane na uraibu kama nilivyofanya mimi na sasa nimekuwa mtu mwenye heshima na ninaeaminiwa tena jamii na familia yangu, Vijana wa Bagamoyo tumieni fursa hii iliyoletwa karibu nanyi, si kama mimi nilitumia gharama kubwa kuifata huduma ya methadone Hospitali ya Taifa Muhimbili kila siku, nawasihi Vijana wenzangu kutokuwa na shaka na matibabu ya methadone, kwani ni matibabu salama na hayana madhara yoyote kwa mraibu aliyeamua kupata matibabu hayo” Ameshuhudia  Bw. Rashid Abdallah

Nae mratibu wa Afya ya Akili na tiba ya dawa kulevya Bagamoyo Bi. Husna Kipilipili akizungumza katika uhamasishaji huo amesema, Methadone ni dawa inayotolewa kumsaidia mraibu aliyeathirika na matumizi ya dawa za kulevya aina ya heroin, matibabu ya methadone humfanya mraibu aache matumizi ya dawa za kulevya bila kupata arosto “withdrawal” na hivyo kuendelea na maisha yake kama kawaida bila matumizi ya dawa za kulevya “heroin”, na dawa hii hutolewa mara moja kwa siku na ipo katika mfumo wa kimiminika yaani “syrup” pia ni dawa ambayo imethibitishwa kisayansi kuwa haina madhara kwa matumizi ya binadamu.




Matangazo

  • TANGAZO LA KUTEULIWA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 AWAMU YA PILI... May 09, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA BAGAMOYO... February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA OBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.. February 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI... July 14, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • HALMASHAURI YA BAGAMOYO YAPANDA MITI 500 ENEO LA MNADA WA ZINGA KUBORESHA MAZINGIRA...

    April 15, 2025
  • TUTAENDELEA KUSIMAMIA KWA DHATI NA HAKI MISINGI YA DEMOKRASIA...

    April 02, 2025
  • ELIMU KUHUSU MPOX YATOLEWA KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI...

    March 20, 2025
  • WAPENI ELIMU WANANCHI KUHUSU UGOJWA WA MPOX...

    March 17, 2025
  • Angalia zote

Video

SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 0733860575

    Simu ya kiganjani: 0733860575

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo