• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Divisheni na Vitengo
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TASAF
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Usimamizi wa Usafi na Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha mawasiliano Serikalini
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2024-2025
      • Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

WATOTO CHINI YA MIAKA MITANO KUSAJILIWA NA KUPATA VYETI VYA KUZALIWA BURE

Posted on: December 3rd, 2019

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Bi. Fatuma O. Latu, leo amefungua rasmi mafunzo kwa wataalamu watakaoendesha zoezi maalumu la uandikishaji na usajili wa watoto wenye umri chini ya miaka mitano ili wapatiwe vyeti vya kuzaliwa bure.

Mafunzo hayo yanayofanyika katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Bagamoyo kwa siku tatu, yameanza rasmi leo na yatakamilika siku ya Alhamisi, huku zoezi la usajili wa watoto ili kupata vyeti vya kuzaliwa likitarajiwa kuanza siku ya Ijumaa tarehe 06/12/2019.

Mafunzo kwa Wataalamu wasajili hao yamelenga kuwajengea uwezo ili kutekeleza mpango wa usajili wa watoto kwa kasi inayotakiwa na kwa ufanisi mkubwa.

“Ni wajibu wenu kuhakikisha zoezi hili mnalitekeleza kwa weledi mkubwa, ili muisaidie Serikali kupata takwimu sahihi zitakazoisaidia kupanga shughuli za maendeleo katika Halmashauri yetu ya Bagamoyo, hivyo umakini mkubwa unatakiwa wakati wa mafunzo ili kupata uelewa sahihi wa kutekeleza zoezi” Amesema Bi. Fatuma Latu

Anaongeza “Kila mtoto ana haki ya kusajiliwa na kupata cheti cha kuzaliwa kwani cheti hiki kina umuhimu mkubwa, ikiwa ni pamoja na kumtambulisha mtoto wakati wa kupata huduma muhimu za kijamii, mfano; wakati wa kuandikishwa shule, kuingia chuo kikuu, wakati wa kujiandikisha ili kupata kitambulisho cha Taifa, kuomba pasipoti ya kusafiria na matumizi mengine mengi muhimu, hivyo ni wajibu wa kila mzazi kuhakikisha anatumia fursa hii kuhakikisha mtoto wake anasajiliwa na kupatiwa cheti cha kuzaliwa”

Jumla ya watoto 14,565 wanatarajiwa kusajiliwa na kupatiwa vyeti vya kuzaliwa kupitia mpango huu maalumu katika Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, ambapo zoezi la usajili wa watoto ili kupatiwa vyeti vya kuzaliwa linatarajiwa kuanza siku ya tarehe 06/12/2019 na litaendelea hadi tarehe 19/12/2019.

Usajili huu wa watoto utafanyika katika Ofisi za Kata zote 11 za Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, pia katika Vituo vya kutolea huduma za Afya, ambavyo ni Zahanati zote, Vituo vya Afya na katika Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo, ambapo Mzazi anatakiwa kufika katika Vituo hivyo vya usajili akiwa na nakala (copy) ya kadi ya kliniki au tangazo la mtoto kuzaliwa ili kufanya usajili huo.

Mpango wa usajili na utoaji vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano katika Mkoa wa Pwani, unatekelezwa na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya watu wa Canada, Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia watoto (UNICEF) pamoja na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA).


Matangazo

  • TANGAZO LA KUTEULIWA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 AWAMU YA PILI... May 09, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA BAGAMOYO... February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA OBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.. February 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI... July 14, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • BAGAMOYO KUJITANGAZA KIMATAIFA SEKTA YA UTALIII...

    May 10, 2025
  • HALMASHAURI YA BAGAMOYO YAPANDA MITI 500 ENEO LA MNADA WA ZINGA KUBORESHA MAZINGIRA...

    April 15, 2025
  • TUTAENDELEA KUSIMAMIA KWA DHATI NA HAKI MISINGI YA DEMOKRASIA...

    April 02, 2025
  • ELIMU KUHUSU MPOX YATOLEWA KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI...

    March 20, 2025
  • Angalia zote

Video

SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 0733860575

    Simu ya kiganjani: 0733860575

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo