• Malalamiko |
    • Wasilina nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Ushauri |
Bagamoyo District Council
Bagamoyo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Muundo wa Taasisi
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Divisheni na Vitengo
    • Divisheni
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Miundombinu, Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TASAF
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Fedha na Hesabu
      • Kitengo cha Usimamizi wa Usafi na Taka
      • Kitengo cha Maliasili na Uifadhi wa Mazingira
      • Kitengo cha Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha mawasiliano Serikalini
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Matangazo
    • Miongozo
    • Fomu mbali mbali
    • Mpango Mkakati
    • Bajeti Kuu ya Halmashauri 2024-2025
      • Bajeti ya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Maeneo ya Uwekezaji
    • Miradi inayoendelea
  • Utalii
    • Kaole Snake Park
    • Kaole Mamba Ranch
    • Caravan Serai
  • Zabuni
    • ZABUNI MBALIMBALI ZA UWAKALA
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao vya Kisheria
    • Vikao vya Wahe. Madiwani
    • Ratiba

WAZIRI WA TAMISEMI AKABIDHIWA MRADI WA UKARABATI MAJENGO SHULE YA MSINGI KAOLE.

Posted on: July 18th, 2021

Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi Tamisemi Ummy Mwalimu amepongeza juhudi zilizofanywa na Taasisi isiyo ya kiserikali ya Lady Fatemah Trust (UK) kwa kuafanya ukarabati wa vyumba 7 vya madarasa,Ofisi ya Mkuu wa shule ,Ofisi ya walimu na ujenzi wa matundu ya choo 2 ya vyoo vya walimu shule  ya msingi Kaole .

Akizungumza wakati wa kukabidhiwa mradi huo amesema kuwa anatambua na anathamini kazi kubwa iliyofanywa kwani wao kama serikali hawatoweza kufanya kila kitu bila kushirikisha wadau mbalimbali wa maendeleo.

‘’Natambua sana kazi kubwa mliyoifanya na ndio maana leo hii nimekuja hapa kwa kuthamini kile ambacho mmekifanya mama keki pamoja na mzee wangu Anuari  ambao wamekuwa wakifanya kazi hizi za jamii kwa Zaidi ya miaka 34 sasa ‘ Waziri Ummy Mwalimu.

Pia Mhe. Ummy  amemshukuru Mbunge wa jimbo la Bagamoyo Mhe Muharami Mkenge kwa kuwezesha kutafuta wadau na kusaidia kufanyika kwa ukarabati wa shule ya msingi Kaole ‘’tunakushukuru sana mhe mbunge na mkurugenzi wa Halmahsuri kwa kufanikisha kuwapata wadau hawa..

Mhe. Waziri pia amevutiwa na hali iliyopo ya majengo kwa ubunifu iliofanyika kwani umeleta taswira nzuri pia itasaidia kupitia ukarabati huo kudumu kwa muda mrefu kwani wametumia ubunifu mzuri wa kutopaka rangi na kuamua kupiga chooping.‘’Kwa hili nipongeze sana na nimepata ushahidi wa kwenda kumuonesha waziri ujenzi na uchukuzi kwamba sasa tutoe huo muongozo mpya wa majengo ya serikali’’amesema Waziri Ummy 

Aidha Mhe. Ummy ametoa wito kwa wadau kushirikiana na serikali kukarabati shule zote ambazo ni kongwe na zina miundombinu ambayo sio rafiki huku pia akisema kupitia Tamisemi tayari swala la ukarabati shule hizo tayari wameliweka kipaombele na tayari wamekwisha anza kukarabati shule kongwe za sekondari na zoezi ilo likimalizika wataanza ukarabati wa shule kongwe za msingi takribani 2100 ambazo zimejengwa kabla ya uhuru.

Sanjari na hayo Mhe. Ummy amesisitiza kuwa upo uhaba wa madarasa katika shule za msingi na sekondari hivyo wanaomba wadau kuendelea kuiunga mkono serikali ili kuhakikisha kuwa wanatatua tatizo lililopo la uhaba wa vyumba hivyo vya madarasa huku kwa mkoa wa Pwani kuna uhaba wa vyumba 4300 na kusema kuwa maelekezo ni kuhakikisha kupitia Wenyeviti wa Halmashauri ,Wakurugenzi  wa Halmashauri wanapeleka asilimia 40 ya fedha wanazokusanywa kwa mapato ya ndani ya Halmashauri kutatua kero za wananchi katika Halmashauri zetu.

Pia amewaomba Wenyeviti wa Halmashauri kuweka swala hilo kama ni kipaombele na kusema kuwa wataichambua hiyo aslimia 40 iliyopelekwa kwenye maendeleo imekwenda kufanya jambo lipi ambalo limegusa wananchi wa Bagamoyo ‘’maendeleo yangu mimi ni kanijengee darasa,kanifanyie ukarabati wa madarasa,kaninunulie madawati watoto wangu wasikae chini,kanijengee vyoo hayo ndio maendeleo kajenge zahanati,nunua vifaa tiba jenga nyumba za walimu kwahiyo nadhani wakurugenzi mmenisikia amesema Waziri Ummy.

Mhe. Ummy amesema kuwa wapo katika mpango wa kujenga vyumba vya madarasa shule ya msingi na sekondari  Zaidi ya elfu kumi  katika Bajeti hii ya mwaka 2021/22 ili kuweza kuwatoa watoto chini ya mti na kwenye misongamano, na kuwatoa watoto kwenye darasa bovu Zaidi ya watoto laki tano.

Halmashauri ya Bagamoyo kupitia ofisi ya mbunge  ilipata ufadhili wa ukarabati wa vyumba 7 vya madarasa,ofisi ya mwalimu mkuu,ofisi ya walimu,na ujenzi wa matundu ya 2 ya vyoo vya walimu kutoka taasisi isiyo ya kiserikali ya ‘’LADY FATEMAH TRUST ( UK).ambapo ukarabati huo umetumia kiasi cha shilingi Milioni 73.


Matangazo

  • TANGAZO LA KUTEULIWA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI KUDUMU LA WAPIGA KURA 2025 AWAMU YA PILI... May 09, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU WILAYA YA BAGAMOYO... February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA YA OBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.. February 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI... July 14, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • BAGAMOYO KUJITANGAZA KIMATAIFA SEKTA YA UTALIII...

    May 10, 2025
  • HALMASHAURI YA BAGAMOYO YAPANDA MITI 500 ENEO LA MNADA WA ZINGA KUBORESHA MAZINGIRA...

    April 15, 2025
  • TUTAENDELEA KUSIMAMIA KWA DHATI NA HAKI MISINGI YA DEMOKRASIA...

    April 02, 2025
  • ELIMU KUHUSU MPOX YATOLEWA KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI...

    March 20, 2025
  • Angalia zote

Video

SOKO LA SAMAKI BAGAMOYO.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Instagram

Tovuti muhimu

  • Salary Slip Portal
  • Presidential Office Regional Administrative and Local Goverment
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)

Wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Free Visitor&Stat Counter

Muongozo wa Ramani

Wasilina nasi

    Bagamoyo

    Anwani ya Posta: Box 59 BAGAMOYO

    Simu: 0733860575

    Simu ya kiganjani: 0733860575

    Barua pepe: ded.bagamoyo@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali
    • Sitemap
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo